Bondia ‘Star Boy’ Ajifua Kumkabili Jibaba

Kocha wa mchezo wa masumbwi nchini Habibu Kinyogoli kushoto akimwelekeza jinsi ya kutupa makonde bondia Shabani Mhamila ‘Star Boy’ katika kambi ya Ilala iliyopo Amana CCM jana Sta Boy anajiandaa na mpambano wake na Yusuph Jibaba utakaofanyika siku ya mei mosi katika ukumbi wa PTA Sabasaba Dar es salaam. (Picha na Super d blog)

Na Mwandishi Wetu

BONDIA Shabani Mhamila ‘Star Boy’ anaendelea kujifua kwa ajili ya kumkabili Yusuf Jibaba katika pambano la utangulizi wakati wa mchezo wa kati ya Francis Cheka na Thomas Mashali. Pambono la raundi nne linatarajiwa kufanyika katika Ukumbi wa PTA Sabasaba, Dar es Salaam Mei Mosi mwaka huu, linatarajiwa kuwa la vuta nikuvute kutokana na kila mmoja kujigamba kujiandaa vema.

Kocha wa Star Boy, Habibu Kinyogoli ‘Masta’ akisaidiwa na Rajabu Mhamila ‘Super D’ wamesema kuwa bondia wao anaendelea vizuri na mazoezi kwa ajili ya  kujiandaa kumchakaza Jibaba ili kuendelea kujiwekea sifa nzuri.

“Bondia wangu yuko katika maandalizi ya kutosha kuhakikisha anafanya vizuri katika pambano hilo la utangulizi kati ya Cheka na Mashali” alisema Super D na kuongeza Star Boy alishawai kuwa bingwa wa masumbwi mwaka 1998 ambapo alisimama kwa kipindi kidogo kutokana na maisha ya nchini lakini kwa sasa ameamua kurudi katika ulingo wa masumbwi ili aweze kutoa changamoto za mchezo huo kutokana na mabondia wengi kutokujua sheria na kanunu za mchezo huo.

Star Boy mwenye rekodi ya; won 14 (KO 5) + lost 7 (KO 4) + drawn 2 = 23 ambaye mkanda wa kwanza wa taifa alichukua kwa kumtwanga Theodor Luanda Frebruary 2,1996 na kutetea vema 10 Februari 1997 kwa kumtwanga bondia Chaurembo Palasa wa Super D.

Kocha huyo wa kimataifa wa mchezo wa ngumi nchini, alisema kuwa katika mchezo huo kutakuwa na DVD za mafunzo ya mchezo huo zenye mapambano makubwa ya mabondia wa ndani na nje ya nchi.