Ujumbe wa Tanzania pamoja na ujumbe wa Benki ya Dunia wakijadili namna ya kuendeleza na kuboresha sekta mbalimbali zilizopewa vipaumbele kwa Tanzania ambavyo ni pamoja na Nishati, Usafirishaji na masuala mazima ya MKUKUTA.
Kutoka kushoto ni Mchumi wa Wizara ya Fedha Bw. Patrick Pima, Naibu Katibu Mtendaji Ofisi ya Rais Tume ya Mipango Prof. Longinus Rutasitara, Afisa Mwambata anayeratibu masuala ya uchumi, biashara na uwezeshaji ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa Bw. Paul Mwafongo wakiandika majadiliano hayo.
Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia kanda ya Afrika Bw. Makhtar Diop aliyekaa katikati, akitoa ufafanuzi wa mikakati wa vipaumbele hivyo. Kutoka kushoto ni Mwakilishi mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier na kulia ni Mkurugenzi wa Sekta ya kupunguza umasikini na masuala ya Uchumi kanda ya Afrika Bw. Marcelo Giugale.
Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Fedha, Dk. Wiliam Mgimwa akitoa ufafanuzi wa vipaumbele kwa ujumbe wa Benki ya Dunia.
Kutoka kushoto ni Mchumi wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Dk. Dickson Lema, Mchumi wa BOT Bi. Haika Mbaga, Kaimu Balozi Ubalozi wa Tanzania Washington DC Bibi Lily Munanka, Kamishna wa Fedha za Nje Wizara ya Fedha Zanzibar Bi. Bihindi Nassor na Mchumi wa BOT Bi. Sauda Msemo wakifuatilia majadiliano hayo.
Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Mipango na Uratibu kanda ya Afrika Bw. Jan Walliser, Meneja wa Social Protection kanda ya Afrika Bi. Lynne D-Sherburne – Benz na baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Dunia wakifuatilia majadiliano hayo.
Wafanyakazi wa Benki ya Dunia wakifuatilia majadiliano.
Wafanyakazi wa Benki ya Dunia wakifuatilia majadiliano.
Kutoka kushoto ni Meneja wa Ubinafsishaji Sekta ya Maendeleo kanda ya Afrika Bi. Irina Astra Khan, Mkurugenzi wa Mipango na Uratibu kanda ya Afrika Bw. Jan Walliser akijibu hoja katika majadiliano hayo. Kulia ni Mwakilishi mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier akisikiliza kwa makini. (Picha zote na Bi. Ingiahedi Mduma na Bi. Eva Valerian – Washington DC)