BENDI maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya “Ngoma Africa Band” imepokea kwa hudhuni na majonzi makubwa taarifa ya kifo cha mwanamuziki mkongwe barani Afrika hayati Bibi Fatuma binti Baraka (Bi.KIDUDE) na kutaka mwenyezi Mungu amrehemu.
Ngoma Africa band inatoa mkono wa pole na rambirambi kwa familia ya marehemu Bi.Kidude, pia kwa Watanzania wote walioguswa na msiba huo, hasa wanamuziki kwa kuondokewa na mkongwe wetu Bi. Fatuma Binti Baraka (Bi.Kidude),ambaye alikuwa ni balozi na hadhina ya utamaduni wa muziki wa mwambao na waswahili, kitaifa na kimataifa.
Marehem Bi. Kidude hakuwa msanii au mwanamuziki tu bali alikuwa mpiganaji jemedari aliyeupigania na kuulinda utamaduni wa jadi ya Kiswahili na muziki wa mwambao.
Bendi ya Ngoma Africa inaungana na watanzania wote wa ndani na nje ya nchi katika kuomboleza msiba huu wa mkongwe wa sanaa barani barani Afrika hayati Bibi. Fatuma Binti Baraka (Bi. Kidude), Ngoma Africa band itasimamisha shuguli za kutumbuiza kwa muda wa siku 10 kuanzia sasa kwa ajili ya maombolezo ya msiba wa marehemu Bi. Kidude.
Mwenyezi mungu amlaze mahala pema peponi Bibi.Fatima binti Baraka (Bi.Kidude)
Amin.