MIKUTANO ya kipupwe imeanza rasmi mjini Washington DC kuanzia Aprili 15, 2013 na kuhudhuriwa na nchi wanachama zaidi ya 188. Waziri wa Fedha Dk. Augustino William Mgimwa ni mmoja wa magavana katika mikutano hiyo akiiwakilisha Tanzania, kama mwanachama.
Kila kunapokuwa na mikutano ya kipupwe maelfu ya wafanyakazi wa Serikali, waandishi wa habari, mashirika yasiyo ya kiserikali, washiriki waalikwa kutoka sekta za elimu na binafsi, wanakutana mjini Washington DC kwa mikutano hii ya kipupwe ya Benki ya Dunia na Shrika la Fedha la Kimataifa.
Wajumbe wengine ambao hushiriki ni pamoja na kamati za kifedha, ambazo zinajadili maendeleo ya kazi za Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa. Mikutano hiyo huambatana na semina na majadiliano mbalimbali, mikutano ya waandishi wa habari na matukio mbalimbali yanayohusu uchumi jumla, maendeleo ya kimataifa na masoko ya kifedha ya kimataifa.
Mikutano ya Shirika la Fedha la Kimataifa na Magavana wa Benki itakuwa kipindi kijacho baada ya mikutano hii. Bodi ya Magavana wa Benki ya Dunia na Bodi ya Magavana wa Shirika la Fedha la Kimataifa kwa kawaida wanakutana mara moja kwa mwaka kujadili kazi zinazohusu taasisi zao.
Mikutano ya mwaka , inayofanyika mwezi Septemba / Oktoba huwa inafanyika mjini Washington DC kwa miaka miwili mfululizo na mwaka wa tatu huwa inafanyika kwa nchi mwanachama. Uzinduzi wa Mikutano hii ya Bodi ya Magavana ilifanyika Sanannah, Georgia, USA mwezi March mwaka 1946. Mkutano wa kwanza wa mwaka ulifanyika mjini Washington DC mwaka 1946.
Katika mikutano hiyo ya mwaka makundi ambayo ni kamati za fedha, kamati za maendeleo, Nchi za kundi la kumi, Nchi za kundi la ishirini na nne na makundi mbalimbali ya nchi wanachama wanafanya majumuisho ya mikutano hiyo na kila kundi linawasilisha makubaliano yao katika mkutano mkuu wa mwaka. Mikutano ya mwaka inakuwa na utangulizi wa mkutano wa siku moja ambapo Bodi ya Magavana wanafanya maamuzi ya namna mambo ya sasa ya Shirika la Fedha la Kimataifa yanatambulika na kupitisha maazimio husika.
Katika Mikutano hiyo ya mwaka, mwenyekiti wake anakuwa Gavana wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa, na uenyekiti huo ni wa mzunguko kati ya nchi wanachama kila mwaka. Kila baada ya miaka miwili wanachagua Wakurugenzi watendaji. Kila mwaka wanakaribisha wanachama wapya kuingia katika shirika la fedha la kimataifa na Benki ya Dunia.
Kwakuwa mikutano ya mwaka inakusanya namba kubwa ya nchi wanachama wanaotambulika rasmi kwa pamoja, wanatoa nafasi ya ushauri mkubwa na mdogo, uliorasmi na usio rasmi. Semina mbalimbali zinafanyika sanjari na mikutano hiyo, ikiwahusisha waendesha semina kwa wanachama ambao ni wafanyakazi na waandishi wa habari.
Mikutano ya mwaka imeweka semina ambazo zitalenga katika makongamano ambayo yanajenga na yanahusisha sekta binafsi, wawakilishi kutoka serikalini na maofisa wakuu kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa na wafanyakazi wa Benki ya Dunia. Somo la fedha za kimataifa ambalo kila mwaka linatolewa kwa na Per Jacobsson kwa ufadhili wa Taasisi iliyoanzishwa kwa heshima ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa, pia inatolewa kila mwaka sambamba na mikutano hiyo.
Mikutano ya mwaka ya Shirika la Fedha la Kimataifa na Benki ya Dunia iliyofanyika nje ya Washington DC kuanzia mwaka 1947—2012
Mwaka Mahali
1947 London
1950 Paris
1952 Mexico City
1955 Istanbul
1958 New Delhi
1961 Vienna
1964 Tokyo
1967 Rio de Janeiro
1970 Copenhagen
1973 Nairobi
1976 Manila
1979 Belgrade
1982 Toronto
1985 Seoul
1988 Berlin
1991 Bangkok
1994 Madrid
1997 Hong Kong
2000 Prague
2003 Dubai
2006 Singapore
2009 Istanbul
2012 Tokyo
Mikutano hii itaendelea hadi mwishoni mwa wiki ijayo na washiriki wengi wanazidi kuingia mjini hapa.
Imetolewa na Msemaji Mkuu, Wizara ya fedha
Bi Ingiahedi Mduma, Washington DC
16/04/2013