Mmoja wa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam akiwa amepanda mkokoteni kuvushwa kutoka upande mmoja wa barabara kwenda mwingine maeneo ya Kariakoo
Wananchi anuai wakivushwa kwa mikokoteni kuepuka kuingia kwenye maji yanayofurika mitaa mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam, hii ni maeneo ya Kariakoo jana.
Mvua jijini Dar es Salaam ni kero kwa kila mmoja. Picha mbalimbali juu zikionesha wananchi wakipambana kukabiliana na kero za kujaa maji barabarani, hii ni eneo la Msimbazi.
Maji kujaa kwenye barabara mitaa mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam ni kitu cha kawaida, hii ni Gerezani, Kariakoo.