KAMBI Mpya ya Miss Utalii Tanzania 2012/13 imeanza kwa kasi mpya Baada ya washiriki Kumi na nne kupata Tuzo za Utalii Tanzania.
Mchakato wa kutoa tuzo hizo mbalimbali ikiwemo za Utalii ulianzia Dar Live Mbagala Dar es Salaam ambapo alipatikana Mshindi wa Tuzo ya Vipaji (Tallent Award) alichukua Miss Utalii Tanzania 2012/13 kutoka mkoa wa Manyara, Baada ya hapo alipatikana Mshindi wa Tuzo ya Uandishi na Mawasiliano ya Umma (SJMC Media Award) iliyofanyika Katika Chuo Kikuu Cha Dar es salaam-Shule kuu ya Uandishi na Mawasiliano kwa uma ambapo ilichukuliwa na Miss Utalii Tanzania 2012 kutoka Mkoa wa Arusha ambaye pia alipata nafasi ya Kusoma katika Chuo hicho.
Mchakato wa kupata Tuzo zengine uliendelea ambapo washiriki Wengine Kumi na nne walipata Tuzo zao, Tuzo mbili za awali ambazo zilichukuliwa na Miss Utalii Tanzania 2012/13 kutoka Mkoa wa katavi alipata Domestic Tourism Award, na tuzo ya pili ilikuwa ni ya National Parks Tourism award ambayo ilichukuliwa na Miss Utalii Tanzania 2012/13 kutoka Mkoa wa Lindi. Tuzo zote hizo zilitolewa katika Hifadhi ya Taifa ya Saadani (Saadani National Park) ambapo pamoja na kutoa tuzo hizo kuliambatana na Burudani kabambe ya ngoma za asili iliyo tolewa na Washiriki wa Miss Utalii Tanzania 2012/13.
Washiriki wa Miss Utalii Tanzania 2012/13 wakiwa katika hifadhi ya Taifa ya Mikumi kutembelea vivutio mbalimbali vinavyo patikana katika Hifadhi hiyo, walifanya tena Show maalum ya Burudani ya Ngoma za asili pamoja na Kutoa Tuzo zengine Kumi na Mbili kwa washiriki Mbalimbali wa Miss Utalii Tanzania 2012/13.
Tuzo ambazo zilitolewa ilikuwa ni pamoja na Mikumi Conference Tourism Award ambayo ilichukuliwa na Miss Utalii Tanzania 2012/13 kutoka Mkoa wa Dar es salaam 2, Cultural Tourism Award ambayo ilichukuliwa na Miss Utalii Tanzania 2012/13 kutoka mkoa wa Simiyu ,Marine Park Tourism Award ambayo ilichukuliwa na Miss Utalii Tanzania 2012/13 kutoka Mkoa wa Mtwara, Forest Services Tourism Award ambayo ilichukuliwa na Miss Utalii Tanzania 2012/13 kutoka kutoka Vyuo vikuu, Mount Kilimanjaro Tourism Award ambayo ilichukuliwa na Miss Utalii Tanzania 2012/13 kutoka Mkoa wa Kilimanjaro,Ngorongoro Crater Tourism Award ambayo ilichukuliwa na Miss Utalii Tanzania 2012/13 kutoka Mkoa wa Dodoma, Sports Tourism Award ambayo ilichukuliwa na Miss Utalii Tanzania 2012/13 kutoka Mkoa wa Tanga, Serengeti Migration Tourism Award ambayo ilichukuliwa na Miss Utalii Tanzania 2012/13 kutoka Mkoa wa Rukwa, Tour Oparator Tourism Award ambayo ilichukuliwa na Miss Utalii Tanzania 2012/13 kutoka Mkoa wa Kagera, Wildlife Tourism Award ambayo ilichukuliwa na Miss Utalii Tanzania 2012/13 kutoka Mkoa wa Morogoro, Bee Keeping Tourism Award ambayo ilichukuliwa na Miss Utalii Tanzania 2012/13 kutoka Mkoa wa Tabora na Community Services Tourism Award ambayo ilichukuliwa na Miss Utalii Tanzania 2012/13 kutoka Mkoa wa Shinyanga.