NCHI ya Afrika Kusini imetangaza kutuma wanajeshi Jamhuri ya Demokrasi ya Congo kuungana katika kikosi maalumu cha Umoja wa Mataifa kilichoingilia kati nchini humo kuwanyan’ganya silaha wapiganaji.
Taarifa ya kupeleka majeshi nchini Congo imetolewa ikiwa ni majuma machache baada ya wanajeshi 13 wa Afrika Kusini kuuwawa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati katika hali ya kutatanisha.
Upande wa upinzani umelaani mpango huo, wanasema kuwa haukufikishwa mbele ya bunge. Waziri kivuli wa Ulinzi wa chama cha Democratic Alliance, David Maynier, alisema kuna hatari ya wanajeshi zaidi kupoteza maisha yao. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilitoa idhini mwisho wa mwezi uliopita kutuma kikosi kitachoweza kupigana na kuingilia kati katika Congo.
-BBC