Waziri Pinda Awaasa Watanzania Kwewnye Harusi ya Mangula
Waziri Mkuu Mizengo Pinda amewataka Watanzania kupendana na kuishi kama watoto wa baba mmoja na kuondoa tofauti za kidini ambazo zinaweza kuliingiza taifa katika matatizo makubwa. Waziri Mkuu katika melezo yake ametolea mfano wa hivi karibuni ambapo baadhi ya Wakristo na Waisilamu walianza kugombana kwa ajili ya uhalali wa kuchinja.
Alisema Watanzania hawana budi kuheshimu imani za wenzao kwani miaka ya nyuma watu walikuwa wakishirikiana kiasi kwamba huwezi kujua tofauti ya Mkristo na Muislamu kwa vile kila mtu alimpenda mwenzake na kuheshimu dini ya mwenzake.
Hivyo amewaomba viongozi wadini kusaidia kurudisha upendo ambao ulikuwepo amesema amefurahishwa na kuona hata viongozi wa dini ya kisilamu Kuwepo kanisani katika ibada ya kubariki ndoa ya Philip Mangula na Bibi Yolanda Kabelege amesema watu wanjombe ndio mfano wakuigwa.
Waziri Mkuu ameyasema hayo alipokuwa amehudhuria sherehe ya kubariki ndoa ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula na Mwalimu Yolanda Kabelege ambayo imefanyika katika Kanisa Kiinjili la Kilutheri mkoani Njombe.
Naye Katibu Mkuu wa CCM, Abdurahamani Kinana aliwapongeaza wana ndoahao kuamua jambo lakufunga ndoa kwani hata vitabu vitakatifu vinasema nyumba iliyo katika ndoa hata mungu huibariki nakuipa amani. Sherehe hiyo imefanyika Jumamosi ya Aprili 6, 2013 na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa dini, Chama na Serikali, mabalozi na wananchi wa Njombe (Picha na Chris Mfinanga)