Wanahabari na Mafunzo ya Sensa Jijini Dar es Salaam

Mhariri wa Habari Msaidizi Stella Nyemenohi kutoka gazeti la Habarileo akitoa maoni yake jinsi waandishi wa habari wanavyoweza kutumia ripoti ya sensa ya watu na Makazi ya mwaka 2012 kupata majibu mbalimbali ikiwa ni pamoja na totauti ya idadi ya watu kati ya mkoa mmoja na mwingine wakati wa mafunzo ya siku moja kwa waandishi wa habari yaliyoandaliwa na ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) leo katika Hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mpiga picha wa kampuni ya New habari (2006) Anthony Siame na kulia ni mwandishi wa Habari wa Televisheni ya Zanzibar (ZBC) Khamisuu Ally.

Mkurugenzi wa Sensa ya watu na takwimu za jamii Ephraim Kwesigabo akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) umuhimu wa kuripoti kwa usahihi taarifa ya Sensa ya watu na Makazi ya mwaka 2012, Idadi ya watu kwa ngazi za utawala, matokeo muhimu wakati wa mafunzo ya siku moja kwa waandishi wa habari yaliyoandaliwa na ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) leo jijini Dar es Salaam.

Mratibu wa Sensa Zanzibar, Mayasa Mwinyi (kushoto) akimuelekeza mwandishi wa habari wa gazeti la Majira Darlin Said (kulia) jinsi ya kutumia takwimu za sensa ya watu na Makazi ya mwaka 2012, Idadi ya watu kwa ngazi za utawala , matokeo muhimu wakati wa mafunzo ya siku moja kwa waandishi wa habari yaliyoandaliwa na ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) leo katika Hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam. Picha na Anna Nkinda – Maelezo

Mwandishi wa Habari wa Televisheni ya Zanzibar (ZBC) Mohamed Ally (kulia) akiuliza swali wakati wa mafunzo ya siku moja ya waandishi wa habari yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam jinsi ya kutumia takwimu za Sensa ya watu na Makazi ya mwaka 2012, Idadi ya watu kwa ngazi za utawala, matokeo muhimu yaliyoandaliwa na ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) . Kushoto ni Mustapha Musa mwandishi wa habari kutoka Zenj FM.
Picha na Anna Nkinda – Maelezo