Mshindi wa Pambano la Omar na Madilu Kucheza Uphilipino
MSHINDI kati ya mabondia ya Issa Omar (peche boy) na Shaban Madilu wanaotarajia kucheza Aprili 7 jijini Dar es Salaam, ambaye pia atatawazwa kuwa Bingwa mpya wa Universal Boxing Organization uzito wa light fly amepata shavu la kwenda kucheza nchini ufilipino.
Bingwa huyo anatarajiwa kupambana na bondia Lienel Legada ambaye ni Bingwa wa uzito huo nchini Ufilipino, mchezo utakaopigwa Mai 18. Pambano hilo litafanyika katika Mji wa Dumaguete, Negros Oriental nchini Uphilipino.
Ofa hiyo imekuja baada ya vyama vya ngumi kupitia record zao na kuwashauri mabondia hao kucheza ubingwa wa UBO (Universal Boxing Organization, ambao pia upo wazi kutokana na bingwa aliepita kutoutetea kwa kipindi kirefu.
UBO kupitia mwakilishi wao Kanda ya Africa Mashariki, Emmanuel Mlundwa imekubali kudhamini pambano hilo kwa kutoa ubingwa huo kwa mabondia wawili toka nchi moja yaani Tanzania kugombea.
Hii ni nafasi ambazo ni mara chache kutokea kupamba nishwa mabondia wa nchi moja, pindi itakuwa na muda mfupi wa kuutete ubingwa huo kwa ofa hiyo ya Ufilipino, ambayo itakuwa ukishirikishwa na ubingwa wa ‘PAN PACIFIC’ lightly weight title nchini Ufilipino mwishoni mwa mwezi ujao.
Hali hiyo pia itazingatia bondia na matokeo ya mpambano wa Aprili 7 utakao fanyika katika Ukumbi wa CCM, Mwinjuma-Mwananyamala. Ni mpambano ambao pia utawakutanisha mabondia wengi wakongwe na chipukizi.