Jukwaa la Afya EAC Lazinduliwa Kigali

Dk. Richard Sezibera

Na James Gashumba, EANA

JUKWAA la Afya la Afrika Mashariki (EAHP), taasisi inayolenga kuwezesha na kuboresha sekta ya afya, ilizinduliwa juzi mjini Kigali, Rwanda huku wito ukitolewa kwa serikali za kanda hiyo kushirikiana na taasisi hiyo kwa manufaa ya jamii. EAHP pia inalenga kuleta maendeleo katika katika taasisi za afya na kuoanisha sera na sheria zinazohusiana na sekta ya afya katika kanda hiyo ya Afrika Mashariki.

Kwa mujibu wa Shirika Huru la Habari la Afrika Mashariki (EANA) jukumu la taasisi hiyo pia ni pamoja na kutoa msukumo kwa sekta binafsi na asasi za kiraia juu ya masuala ya afya na wataalamu wamasia kutoka nchi wananchama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC). Akizindua taasisi hiyo, Naibu Katibu Mkuu wa EAC anayeshughulikia Tija na Sekta ya Jamii, Jessica Eriyo alisema juhudi hizo zitasaidia kuboresha sekta ya afya katika kanda.

“Tunahitaji watu wenye afya na wazalishaji ambao wananufaika na ubora na unafuu wa huduma za afya katika kanda.Hii tu si kwamba inaendana na mkakati wa EAC lakini pia inaendana na mikakati ya sasa ya maendeleo ya Afrika Mashariki,” alisema.

Alisisitiza umuhimu wa serikali kushirikiana na sekta binafsi kuunga mkono juhudi hizo ili kushughulikia changamoto zinazoikabili sekta ya afya.

Eriyo alitoa wito wa kuwepo kwa kampeni zaidi kuelimisha wananchi juu ya masuala ya afya katika ngazi za chini kabisa ambako asilimia 70 ya magonjwa yanayowasumbua raia yanaweza kuzuilika. Mwenyekiti wa EAHP, Dk. Amit Thakker pia alibainisha kwamba watu wengi bado wanaugua magonjwa ambayo yanaweza kuzuilika.

“Tunataka kuzindua kwanza jukwaa hili na halafu tuone kitakachofuata katika kushughulikia changamaoto zinazoikabili sekta hii kwa kupeana taarifa na kufanyakazi kwa pamoja katika,” alisema Thakker.