Hoteli ya Double Tree Yaipiga ‘Tafu’ Shule ya Msingi Mikocheni “A”

Meneja Mkuu wa Hoteli ya DoubletTree by Hilton Bw. Sven Lippinghof (katikati) na Mkurugenzi wa Masoko wa Hoteli hiyo Bw. Florenso Kirambata (kulia) kwa pamoja wakimkabidhi moja ya boksi zenye taa zinazotumia nishati ya Jua Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mikocheni A Salehe Mwakwiro ikiwa ni muendelezo wa kampeni ya matumizi ya nishati ya jua ambayo itadumu kwa muda wa miaka miwili katika shule za mkoa wa Dar es Salaam.


Meneja Mkuu wa Hoteli ya DoubletTree by Hilton Bw. Sven Lippinghof aliyeambatana na Mkurugenzi wa Masoko wa Hoteli hiyo Bw. Florenso Kirambata akisaini kitabu cha wageni katika Shule ya Msingi Mikocheni A walipowasili shuleni hapo kuendeleza kampeni ya matumizi ya taa za nishati ya jua ambayo itadumu kwa muda wa miaka miwili katika shule za mkoa wa Dar es Salaam. Kushoto ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Salehe Makwiro.

Mkurugenzi wa Masoko wa Hoteli hiyo Bw. Florenso Kirambata akitia saini kitabi cha wageni katika shule hiyo.

Mkurugenzi wa Masoko Hoteli ya DoubleTree by Hilton Florenso Kirambata (kulia) akitoa somo ya matumizi ya taa zinazotumia nishati ya Jua ambazo pia ni rafiki wa mazingira kwa Wanafunzi wa darasa la Saba wa Shule ya Msingi Mikocheni A na kuwaasa kuepeuka kutumia vibatari muda wa kujitosema ambavyo vimekuwa vikisababisha majanga ya kuungua kwa watoto wengi nchini. Kushoto ni Meneja Mkuu wa Hoteli hiyo Bw. Sven Lippinghof.

Baadhi ya wanafunzi wa darasa la saba wa Shule ya Msingi Mikocheni A wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Masoko Hoteli ya DoubleTree by Hilton Florenso Kirambata (hayupo pichani) wakati akiwapa somo la matumizi ya taa zinazotumia Nishati ya Jua ambazo pia ni rafiki wa Mazingira.

Mkurugenzi wa Masoko Hoteli ya DoubleTree by Hilton Florenso Kirambata akitoa maelekezo jinsi ya kutumia taa hizo kwa wanafunzi wa darasa la saba wa shule hiyo.

Mkurugenzi wa Masoko wa Hoteli hiyo Bw. Florenso Kirambata akiwaonyesha mwanga wa taa hizo za nishati ya Jua ambazo ni imara na zinadumu kwa muda wa miaka 10 na zenye uwezo wa kutumika masaa 4 mpaka kuisha chaji yake.

Wanafunzi wa Darasa la Saba katika shule msingi Mikocheni A wakati wa hafla ya kukabidhiwa taa zinazotumia Nishati ya jua ambazo zimetolewa na Hoteli ya DoubleTree by Hilton. Wanafunzi hao wameishukuru Hoteli hiyo na kusema taa hizo zitawasaidia kujisomea hata kipindi ambacho Umeme umekatika majumbani hivyo kuongeza uwezo wao kielimu.

Kampeni hiyo Hoteli ya DoubleTree by Hilton itakuwa ikigawa taa 200 za mezani zenye kutumia nishati ya jua kwa wanafunzi wa darasa la saba kwa shule tofauti kila mwezi, lengo likiwa nikuwafanya wawe na ufahamu zaidi juu ya chanzo kingine cha umeme ambacho ni rafiki wa mazingira kwa kupitia mafunzo katika madarasa yao.