BONDIA mbavu nene Ramadhan Kido anataka tena kuzichapa na mwenzake Alphonce Mchumiatumbo warudiane baada ya pambano lao la mwanzo lilofanyika uwanja taifa kuchapwa amepania kulipa kisasi.
”Mchumiatumbo amenifanya nimeshindwa kulala kwa muda mrefu nikimfikiria yeye kanipigaje…jibu sipati, nimeamua kurudi tena ulingoni kwa kujipima na Musa Mbabe Aprili 7, 201 CCM Mwinjuma, Mwananyamala Dar es Salaam.” Alisema.
Alisema anatambua kuwa Musa ni bondia mzuri lakini hawezi kupoteza mara mbili mfululizo mapambano yake kitendo ambacho kitamshushia adhi. “Huu ni mwiko wangu nitahakikisha nafia ulingoni na ntajituma kwa nguvu zangu zote na kuhakikisha nampiga KO’ mbaya, kwani siku hiyo sitakuwa na huruma hata kidogo.
Alijitamba kuwa katika mpambano huo lolote laweza kutokea hata ikiwa mtu kupokea kipigo hadi kupoteza uhai. “Hali hii ikitokea sawa tu nina uchungu sana na ngumi na nataka nimuoneshe Mchumiatumbo nakuja kivingine, na nikipigwa katika pambano hilo ni bora niache ngumi,” alisema bondia huyo.