Ziara ya Dkt Shein Chakechake

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dk.Ali Mohamed Shein,akipokea zawadi ya Samli na Siagi kutoka kwa
Mjasiriamali wa Ufugaji wa Ngombe wa maziwa katika shehia ya
Wesha,kijiji cha Kaole Omar Ahmed Omar,katika hafla ya sherehe ya
uzinduzi wa Umeme katika kijiji cha Kilindi jana,[Picha na Ramadhan
Othman,Ikulu.]

Sheha wa Shehia ya Kilindi Abuu Abrahmani
Salum,alipokuwa akitoa shukurani zake kwa Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,kwa kufika
katika kijiji hicho kuzindua Nishati ya Umeme kijijini hapo na
wananchi kuweza kuondokana na tatizo lililowakabili kwa kipindi
kirefu,Rais yupo katika ziara ya kikazi kwa Mkoa wa Kusini
Unguja.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

ais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) akiwa na ujumbe wake wakiangalia
Transfoma ya Umeme katika kijiji cha kilindi Wilaya ya Chake
chake,alipofika kuzindua Umeme kijijini hapo jana,akiwa katika ziara
ya katika Mkoa wa Kusini Pemba.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]