JK Mgeni Rasmi Maadhimisho ya Miaka 25 ya Hospitali ya Kairuki

Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Waziri Mkuu Mstaafu, Dkt Salim Ahmed Salim
wakiangalia watoto wachanga waliotunzwa katika chumba maalum muda mfupi baada ya kuzaliwa wakati Rais Kikwete alipotembelea sehemu mbalimbali
za hospitali ya Kumbukumbu ya Hubert Kairuki akiwa mgeni rasmi katika sherehe za miaka 25 ya kuanzishwa kwake Machi 16, 2013.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongozi wengine wakikata utepe kuzindua rasmi hosteli ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki wakati wa sherehe za miaka 25 ya hospitali ya Hubert Kairuki Mikocheni, Dar es salaam, leo Machi 16, 2013

Msanii Mrisho Mpoto akiburudisha wakati wa sherehe za miaka 25 ya hospitali ya Hubert Kairuki Mikocheni, Dar es salaam, leo Machi 16, 2013

Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi, Waziri Mkuu Mstaafu Dkt Salim Ahmed Salim, na viongozi wa hospitali ya Hubert Kairuki wakiwa katika picha ya pamoja na vijana waliozaliwa
katika hospitali hiyo miaka 25 iliyopita leo Machi 16, 2013.