
Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB Dk. Aloyce Nzuki akiwa katika mazungumzo na Rica Rwigamba Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii nchini Rwanda wakati alipokutana katika maonyesho ya dunia ya Utalii ITB yanayofanyika kwenye jengo la Messe Berlin jijini Berlin Ujerumani, Monesho hayo yanahusisha makampuni yenye kutoa huduma mbalimbali za utalii duniani ambao hukutana na kutangaza utalii wa nchi zao huku wakifanya makubaliano na kuingia mikataba mbalimbali ya kuuziana bidhaa za kitalii, Maonesho hayo yanamalizika rasmi leo.
Mkurugenzi wa Kampuni ya ndege ya Flightlink Capt. Munawer Dhirani akizungumza na Ibrahim Mussa Mkurgenzi wa Utalii Wizara ya Maliasili na Utalii katikati ni Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Christopher Mvula akisikiliza kwa makini wakati Balozi huyo alipotembelea katika banda la Tanzania kwenye maonesho ya ITB yanayomalizika leo jijini Berlin Ujerumani kulia ni Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB Dk. Aloyce Nzuki.
Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Christopher Mvula akizungumza jambo na Mkurugenzi wa Kampuni ya ndege ya Flightlink Capt. Munawer Dhirani wakati walipokutana katika maonesho hayo.
Huu nao ulikuwa ni utalii wa aina yake katika maonyesho hayo ambapo watu mbalimbali walikuwa wakipiga nao picha kwa ajili ya kumbukumbu zao. (PICHA ZOTE NA FULLSHANGWEBLOG)