Richards Commey Kuwania ubigwa wa Dunia Uzito mwepesi April 28, 2013

IBF imempatia Richhard Commey nafasi ya kuwania ubingwa wa dunia kwa vijana katika uzito mwepesi mpambano ambao utafanyika tarehe 28 mwezi wa Aprili mwaka huu.

RICHARDS Commey amedhihirisha uwezo wake wa upigana ngumi wakati alipomtoa kwa TKO bondia Bilal Mohammed na kutangazwa kuwa Mfalme wa uzito mwepesi katika bara la Afrika. Mpambano huo ulifanyika katika ukumbi wa Wills Gym City Engineers katika viunga vya Jamestwon, jijini Accra, Ghana na kuhudhuriwa na wapenzi wengi wa ngumi wakiongozwa na viongozi waandamizi wa Chama cha Ngumi cha Ghana (GBA), viongozi wa Kamati ya Olympic ya Ghana, Meya wa jiji la Accra, pamoja na wWaziri wa Michezo wa Ghana.

Mpambano huo ulianza kwa mbwebwe za aina yake baada ya mabondia wote kuwasili kwenye ulingo wakisindikizwa na mashabiki wao waliokuwa wanacheza ngoma mbalimbali za makabila ya Ghana.

Bilal alianza mpambano katika raundi ya kwanza akikurupuka kutoka kwenye kona yake kama faru na kumfuata Richard kwa nia ya kumsimamisha katika raundi ya kwanza lakini Richard aliweza kuhimili shambulio hilo na kuanza kutoa dozi kwa Bilal.

Katika raundi ya 4 Richard alimpeleka Bilal kwenye sakafu ya ulingo mara mbili kwa ngumi zilizokuwa nzito. Bilal aliweza kuendelea na pambano baada ya kuhesabiwa mara 8! Mashabiki wengi aliuzingira ulingo wakati wote wa mpambano huku wakipiga makalele na ngoma zilizoashia kuwa wawili hao kweli wametawala nyoyo za mashabiki wengi wa ngumi katika nchi ya Ghana.

Mambo yalifikia tamati katika raundi ya saba wakati Richard aliporusha ngumi tatu mfululizo za mchanganyiko na kumpeleka Bilal chini kwa mara ya tatu. Bilal aliamka kwa shida wakati mahesabu ya refarii yalipokuwa yanafikia mwisho na alianza kupepesuka huku refarii akimdaka ili asianguke tena na kuashiria mwisho wa mpambano huo.

Huu ni wakati ambapo Richard Commey alipotangazwa kuwa Mfalme wa uzito mwepesi katika bara la Afrika na ukumbi mzima kuzizima kwa nderemo na shangwe. Kwa ushindi huo, IBF imempatia Richhard Commey nafasi ya kuwania ubingwa wa dunia kwa vijana katika uzito mwepesi mpambano ambao utafanyika tarehe 28 mwezi wa Aprili mwaka huu.