Habari zilizotufikia mitamboni muda si mrefu, ni kwamba yule Rais machachari wa Venezuela kule America ya kusini amefariki dunia kutokana na ugonjwa wa saratani. Rais Chavez alikuwa anasumbuliwa na saratani kwa muda mrefu, na alikuwa akipelekwa Cuba kwa matatibabu mara kwa mara. Rais Chavez alifanikiwa kwa kiasi kukubwa kufanya ugonjwa wake siri na mapaka anafariki haikuweza kufahamika ni saratani ya nini haswa ilikuwa ikimsumbua.
Wavenezuela wapo kwenye masikitiko makubwa kwa kuondokewa na kiongozi wao shujaa, na mpaka sasa haijafahamika ni nani haswa atakuwa mrithi wake, ingawa siku chache kabla hajafa, Chavez alikuwa amempendekeza makamu wake wa Rais, Nicolas Maduro kama mrithi wake.
Source: Associated Press (AP)