Mpambano wa Ubingwa wa Ngumi WBF Kufanyika Mkwakwani Tanga

Bondia Alan Kamote


PAMBANO la masumbwi kutetea mkanda wa mabara wa WBF (World Boxing Forum) unategemea kufanyika katika uwanja wa mkwakwani jijini Tanga kwa kuwakutanisha mabondia, Alan Kamote, ambae ni bingwa mtetezi wa mkanda huo aliouchukua nchini Malawi kwa kuzipiga na bondia Jumanne Mohamed wa Tanga ambae anavyo vigezo na sifa zote za kuugombania ubingwa huo.

Jumanne Mohamed ambae alipata nafasi ya kugombania ubingwa wa dunia nchini Namibia na kuipoteza kwa kupigwa na mnamibia nafasi hiyo imejirudia tena, safari hii katika ubingwa wa mabara na kuugombania katika ardhi ya nchini mwake.

Muandaaji wa pambano hilo Ally Mwanzoa akizungumza na viongozi wa ngumi nchini pamoja na Katibu Mkuu wa ngumi za kulipwa Ibrahim Kamwe amesema ameamua kuandaa pambano hilo ili Alan Kamote autetee mkanda wake alioupata Mjini Blantaya nchini Malawi usije ukapotea kwa kutokuutetea ubingwa wake huo.
Amefikia hatua hiyo baada ya kukaa na uongozi wa ngumi kwa kuangalia bondia gani anafaa na ikaamuliwa Jumanne Mohamed anafaa kutokana na sifa alizonazo na upinzani walionao mabondia hao utaleta mshawasha na msisimko mkoani Tanga, kwa hiyo haina haja ya kumleta mtu kutoka nje ya nchi. Mwanzoa aliendelea kwa kusema pia kutakuwa na mapambano mengine ya utangulizi kati JJ Ngotiko na Haji Juma wa Tanga katika pambano la raundi 10 na kutakuwepo na mapambno mengine mengi ya utangulizi.