Wakina Mama Manispaa Sumbawanga Wamzawadia Mama Salma Kimila

Mke wa rais Mama Salma Kikwete akipokea zawadi kutoka kwa baadhi ya vikundi vilivyoshiriki katika shughuli ya kukabidhi pikipiki kwenye vituo vya afya vya mikoa ya Rukwa na Katavi zilizofanyika huko Matai wilayani Kalambo Mkoani Rukwa tarehe 26.2.2013.

Akiwa amevalia vazi la asili la akina mama wa kabila la Wafipa, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete anashiriki kucheza ngoma ya kabila hilo kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga tarehe 15.2.2013.

Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo Mama Salma Kikwete akipokea zawadi za kimila za kabila la Wafipa, wakati alipokutana na akina mama wa manispaa ya Sumbawanga kwenye ukumbi wa Manispaa hiyo tarehe 25.2.2013.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi ambaye pia ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizindua rasmi shina la wakereketwa la kikundi cha akinamama cha Upendo kilichoko katika makao makuu ya wilaya ya Kalambo katika mji wa Matai tarehe 26.2.2013. Akinamama hao wapatao kumi hujishughulisha na kazi ya kukamua mafuta ya alizeti. PICHA ZOTE NA JOHN LUKUWI-Maelezo