Chakula cha Jioni na Wajumbe wa Oman Zanzibar

Viongozi wa Ujumbe wa Serikali ya Watu wa Oman wakichukua chakula wakati wa hafla maalum kilichoandaliwa kwa ujumbe huo, katika Hoteli ya Serena Mjini Zanzibar jana.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman, Yussuf bin Alawi bin Abdullah akichukua chakula wakati wa hafla maalum kilichoandaliwa kwa ujumbe wa Serikali ya Watu wa Oman ulioongozwa na Waziri Yussuf katika Hoteli ya Serena Mjini Zanzibar jana.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Mwinyihaji Makame Mwadini (kushoto) alipokuwa akitoa hutuba fupi ya kuwashukuru wageni wa ujumbe wa Serikali ya Watu wa Oman ulioongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman Yussuf bin Alawi bin Abdullah (kulia) baada ya kushiriki katika hafla ya chakula maalum katika Hoteli ya Serena Mjini Zanzibar jana.