Kampuni ya Airtel Yatoa Vifaa Mpinga Cup

Meneja Uhusiano wa Airtel bw Jackson Mmbando akikabithi Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani SACP. Mohamed Mpinga mipira itakazotumika katika michuano ya mpinga cup itakayoshirikisha waendasha pikipiki maarufu kama Bodaboda yenye lengo la kutoa elimu ya usalama barabarani . wadhamini wengine wa Mping cup ni pamoja na Rotary Dar es Saalm, Home shopping center pamoja na Mr Price. wakishuhudia katikati ni Meneja uendeshaji Home shopping center Yahaya Zuludi na kulia Mwakilishi wa Mr. Price Sudhirm Maharaj. makabidhiano yamefanyika leo katika ofisi kuu ya trafiki Dar es salaam.

Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani SACP. Mohamed Mpinga zitakazotumika katika katika michuano ya mpinga cup itakayoshirikisha waendasha pikipiki maarufu kama Bodaboda.

KAMPUNI ya Airtel kwa kushirikia na Rotary club, Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mr.Price, Home Shopping Center pamoja na Jeshi la polisi kupitia Kikosi cha Usalama Barabarani imeibuka na mpango wa kipekee kupitia mchezo wa mpira wa miguu kwa madereva wa bodaboda utakaowakutanisha pamoja waendesha boda boda wa jijini Dar es salaam ili kuimarisha uelewa wao wa matumizi ya barabara kwa lengo la kuendelea kudhibiti ajali za barabarani pamoja na elimu ya Polisi jamii.

Akiongea kwa niaba ya Airtel, Meneja Uhusiano wa Airtel Bw, Jackson Mmbando alisema “Airtel tumeona ni vyema kuendeleza ushirika wetu na Jeshi la Polisi usalama Barabarani wakati wote wa mwaka ili kuhakikisha usalama barabarani unazingatiwa”.Udhamini wetu katika mashindano haya ya waendesha Bodaboda una lengo la kulinda afya za Watanzania wanaotumia usafiri wa boda boda, kupitia ushiriki wetu tutafikisha ujumbe na elimu kwa watumiaji wa barabara kwa kuwa michezo inaleta hamasa, inaleta burudani, inafanya mwili kuwa imara hivyo kufikiri vyema, hivyo basi ni matumaini yetu baada ya wiki nzima ya mashindano ya mpira wa miguu washiriki hawa pia wataweka kukumbuka ya waliojifunza muda kwa kipindi cha wiki nzima kwa kutii sheria bila shuruti wanapofanya shughuli zao” aliongeza Bw. Mmbando

Naye Mwakilishi wa Mwakilishi wa Rotary club Dar es Saalam Vinay Choudary alisema “Tumejipanga kupitia michuano hii kusambaza ujumbe juu ya athari kubwa inayoweka hatarini maisha ya waendesha pikipiki. Tunaamini elimu ya kutosha ikitolewa kwa vijana wetu wanaofanya biashara za usafiri kwa njia ya pikipiki kutawaepusha na athari hizi si tu kwa madereva bali kwa abiria na watumiaji wa usafiri huu kwa ujumla.

Kwa upande wake Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani SACP. Mohamed Mpinga akizungumziazoezi hili aliwashukuru wadau hao kwa kuunga mkono jitihada za serikali za kuhakikisha ajali za barabarani zinapungua kwa asilimia tano (10%) mwaka huu.

“Tunaendelea na mikakati mbalimbali tuliojiwekea katika kuhakikisha tunapunguza ajali za barabarani nchini. Mashindano haya ya waendesha Boda boda ni moja ya njia tunayoitumia ya kuwafikia walengwa na kutoa elimu kwa waendesha pikipiki” alisema Kamanda Mpinga.

“Hii ni nafasi ya kipekee kwetu kuwaweka watumiaji wa barabara karibu ili tuweze kufikia malengo yetu” alisisitiza kamanda Mpinga. Takwimu zinaonyesha kuwa mwaka 2012 kulitokea ajali za pikpiki 5763, vifo 930 na majeruhi 5532. Hili ni ongezeko la ajali kwa 7.0%, upungufu wa vifo kwa 1.6% na ongezeko la majeruhi kwa 0.5% ikilinganishwa na mwaka 2011 ambapo kulitokea ajali za pikipiki 5384 zilizosababisha vifo 945 na majeruhi 5506. Kiwango hiki nikikubwa na kimeleta maafa na hasara kubwa kwa jamii na taifa kwa ujumla. Tunawashukuru sana Airtel , Rotary club, Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mr. Price, Home Shopping Center wadau kwa kuendelea kushirikiana nasi kuhakikisha tunapunguza kabisa tatizo hili.Pia tunawashukuru wachezaji kwa timu zao waliojitokeza kupata elimu na kushiriki mashindano haya kuanzia awamu ya kwanza hadi sasa.

Mashindano haya yanatarajiwa kutimua mbio kuanzia tarehe 28/02/2013 katika viwanja vya Polisi Oysterbey kwa kushirikisha timu 8 zote kutoka wilaya ya kinondoni ambapo ni muunganiko wa wacheza soka ambao ni waendesha pikipiki toka vituoni (vijiwe ) vya kinondoni. Mpinga Cup itaendelea katika mikoa ya Kipolisi ya Ilala na Temeke na hatimaye kutafuta mshindi wa mkoa wa Dsm. Kampeni hizi za Usalama barabarini zitaendelea mfululizo hadi mwisho wa kilele cha maadhimisho ya Wiki ya nenda kwa usalama barabarani hapo mwezi September/Octoba 2013.