Mabondia Agbeko na Mendenez Kugombea Ubingwa wa Dunia

Mabondia Agbeko na Mendenez Kugombea Ubingwa wa Dunia

KUNA hekaheka nyingi kwenye jiji la Accra, nchini Ghana wakati wa pambano la kugombea ubingwa wa dunia kati ya bondia marufu Joseph Agbeko kutoka Ghana na Luis Mendenez bondia anayetoka katika nchi ya Amerika ya Kusini ya Columbia watakapokutana siku ya jumamosi tarehe 8 Machi.

Kati ya mapambano ya utangulizi bondia anayeinukia kwa kasi Richard Commey atakutana na bondia mwenzake wa Ghana Bilal Mohammed kugombea mkanda wa IBF Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati (IBF AMEPG) katika uzito mwepesi (Lightweight).

Wawili hao wanatoka katika kambi mbili zinazohasimiana kwa siku nyingi na mpambano wao unategemea kuwa wa kasi, ufundi na wenye kusisimua katika raundi zote 12.

Mpambano wa Richard Commey (khttp://www.youtube.com/watch?v=IBG5a9LtIhU) na Bilal Muhammed umekuwa gumzo kubwa katika jiji la Accra pamoja na majiji mengine katika Afrika ya Magharibi. Hii inatokana na umaarufu wa promota na meneja wa Ruchard Commey Mghana Michael Amoo Bediako anayeishi barani Ulaya akiwa na makazi yake nchini Uingereza kuwa mtu aneyeshughulika na mabondia wenye vipaji vya hali ya juu.

Richard Commey atapenda kuwadhihirishia wapenzi wake kuwa yeye ndiye Mfalme wa Afrika katika uzito wa mwepesi (Lightweight) na hakuka atakayeweza kumzuia katika mipango yake ya kupanda ngazi. Naye Bilal Muhammad atapenda kuudhihirisia ulimwengu kuwa sio bondia anayeweza kusukumwa sukumwa na kwamba ubingwa wa IBF AMEPG katika uzito wa Lightweight na wake.

ISSUED BY: INTERNATIONAL BOXING FEDERATION AFRICA (IBF/AFRICA) DAR-ES-SALAAM, TANZANIA