MLINDA mlango mpya wa kimataifa wa timu ya Azam FC Obren Cucovick kutoka Serbia ameanza mazoezi na klabu yake mpya ya baada ya kutua nchini majuzi akitokea kwao, alipokwenda kwa ajili ya kujindaa na heka heka za mashindano ya Ligi kuu Tanzania bara inayotarajiwa kunaza kutimua vumbi mwezi Agosti.
Jambo Leo ilishuhudia kipa huyo jana akiwa ameanza mazoezi kwa mara yake ya kwanza katika timu ya Azam, kwenye uwanja wao mpya uliopo nje kidogo ya Jiji la dar e Salaam maeneo ya Chamazi jirani na kitongoji maarufu cha Mbagala, ambapo katika mazoezi hayo alianza kwa kuonyesha umahili mkubwa wa kuzua michomo mikali ya washambuliaji wa timu hiyo.
Akizungumza katika mazoezi hayo kiti meneja wa timu ya Azam Khamis Jaffer alisema kuwa, milinda mlango huyo kutokea Serbia alitua nchini juzi akitokea kwao, ambapo jana ndio alianza rasmin kutumua vumbi akiwa na kikosi cha Azam kilichoanza mazoezi huku wakiwa hawajakamilka vyema kutokana na wachezaji wengi kutoripoti mazoezini kwa sababu mbalimbali.
Khamis alisema hata hivyo wanatarajia kufikia wiki ijayo takribani wachezaji wengi watajiunga na wenzao katika mazoezi ya pamoja, ambapo alifafanua kwa sasa kutokana na kutokamilika wamekuwa wakifanya mazoezi ya viungo yaani GYM pamoja na uwanjani mpaka hapo watakamilika kutoaka na idadi ya wachezaji waliosajiliwa msimu huu.
Meneja huyo alisema hata hivyo kwa idadi kubwa ya wachezaji walioripoti mazoezi tayari wameshaanza kuchangamka na mazoezi ya yameshaanza kuonyesha sura ya upinzani uwanjani kutokana na kila mmoja kutaka kuonyesha uwezo wake, ili kumvutia kocha katika kusaka namba katika kikosi cha kwanza.
|Hata hivyo alisema ya kwamba wachezaji wageni walioripoti mazoezi wamevutiwa na uwanja, na kuahidi kujituma zaidi katika kuonyesha viwango vyao vya kandanda ili timu itakapoanza mshikemshike wa Ligi kuu waweze kufanya vyema mapema ili kujiweka katika nafasi nzuri yakupigia ubingwa ambao wameukosa kwa asilimia ndogo katika msimu uliopita.