Kingkapita Aachia Kibao ‘Kuna Tatizo Kwani’?

Kingkapita Aachia Kibao ‘Kuna Tatizo Kwani

MSANII Kingkapita kutoka nchini Tanzania ameachia wimbo wake mpya unaojulika kwa jina la Kuna Tatizo Kwani?. Wimbo huo ambao amemshirikisha msanii Godzilla na kuandaliwa na studio ya DEFATALITY anatarajia kushika wapenzi wengi wa miondoko hiyo.

Katika taarifa yake kwa mitandao ya kijamii msanii huyo amesema wimbo mpya umebeba mistari ya kuelimisha na kuburudisha jamii katika makundi tofauti. Wimbo una mistari kama Baba jambazi, mama changudoa, mtoto kazaliwa konda…otea nini kitafuatia”. //HII BAHATI HAIZIMWI KWA MIDOMO FORM SIX ALIPATA ZIRO NA LEO NDO BOSS WAO// “KUNATATIZO KWANI”.

Alisema wimbo huo unatoa mafunzo na kuwapa moyo watu wanaotafuta na kukumbana na vikwazo mbalimbali na kuwataka wasikate tamaa. //MI MKRISTO WEWE MWISLAM HAIJALISHI DINI GANI TUDUMISHE HII AMANI// “KUNATATIZO KWANI”

Vibao vingine vya Kingkapita ni pamoja na: 1.MTOTO MLITO, 2.MTOTO WA FISADI, 3.SHIKAMOO PESA

Zaidi zama hapa; http://www.hulkshare.com/n8iouqb6fbi8