Mgeni rasmi katika mahafali ya 20 ya Kidato cha Sita ya Shule ya Sekondari St. Anthony Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akizungumza na uongozi wa shule hiyo kabla ya kuanza rasmi kwa sherehe hizo.
Padri akiendesha ibada wakati wa mahafali hayo.
Mgeni rasmi Mstahiki Meya Jerry Silaa akifuatilia ibada hiyo kubariki mahafali ya 20 ya kidato cha sita ya Shule ya Sekondari St. Anthony. Kushoto ni Makamu Mkuu wa Shule hiyo Sylvester John na Mkuu wa shule hiyo Bro. Ismail Edward ( wa pili kulia).
Baadhi ya Wahitimu wa Kidato cha Sita shule ya St. Anthony wakisikiliza mahaburi wakati wa ibada hiyo.
Mgeni rasmi Mstahiki Meya Jerry Silaa akishiriki kwenye sala maalum wakati wa ibada hiyo.
Baadhi ya wahitimu wa kidato cha sita wakisoma sala za mtu mmoja kuombea mambo tofauti ikiwemo Amani kwa Taifa.
Baadhi ya wahitimu wa Kidato cha Sita shule ya Sekondari St. Anthony wakimwogoza mgeni rasmi kwa madoido ya aina yake wakati wa mahafali hayo.
Mgeni rasmi Mstahiki Meya Jerry Silaa akiwasili katika viwanja vya shule ya Sekondari St. Anthony akiwa ameambatana na viongozi wa shule hiyo tayari kuanza rasmi sherehe za mahafali hayo.
Baadhi ya wahitimu wa kidato cha sita wakishiriki kuimba wimbo wa shule.
Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha tano wakiimba wimbo wa kuwaaga dada zao na kaka zao mbele ya mgeni rasmi wakati wa mahafali hayo.
Wanafunzi wa shule ya sekondari St. Anthony wakifanya igizo la Dr. Livingstone lililowavunja mbavu wazazi na mgeni rasmi.
Mgeni rasmi Mstahiki Meya Jerry Silaa akiwa hoi kwa kucheka kutokana na igizo la Dr. Livingstone. Kushoto ni Makamu Mkuu wa pili wa Shule hiyo Rempta Adams akifuatiwa na Mkuu wa Shule hiyo Bro. Ismail Edward.
Makamu Mkuu wa pili wa Shule ya sekondari St. Anthony Rempta Adams akisoma taarifa ya shule hiyo mbele ya mgeni rasmi Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala ambapo amezungumzia changamoto mbalimbali zinazoikabili shule hiyo ikiwa ni pamoja na uhaba wa vifaa vya kufundishia na kujifunza, mabadiliko ya mara kwa mara ya Mitaala na matamko juu ya Elimu, tabia ya wanafunzi kuiga tamaduni za Ughaibuni na Ukosefu/kukatika kwa nishati ya Umeme.
Sehemu ya wazazi na walezi waliohudhuria mahafali hayo.
Makamu Mkuu wa pili wa Shule ya sekondari St. Anthony Rempta Adams akikabidhi taarifa ya shule yake kwa mgeni rasmi.
Makamu wa Rais wa Wanafunzi wa St. Anthony Jacqueline Ndunguru akimkabidhi mgeni rasmi risala hiyo.
Mwanfunzi Samwel Mwanzini akionyesha kipaji chake cha kuimba na kupiga kinanda ambapo alishangaza wengi kwa uwezo aliokuwa nao.
Mwanfunzi Tracy Raymond Ndanshau wa kidato cha tano PCM akiimba sambamba na Mwl. Nikiza Bwenge katika mahafali ya 20 ya kidato cha sita.
Makamu Mkuu wa Shule hiyo Sylvester John (kulia) akisoma risala fupi ya kukabidhi wahitimu kidato cha sita 2013 kwa wazazi rasmi Bw. na Bibi Amos Bujiku wakati wa mahafali hayo.
Wazazi rasmi Bw. na Bibi Bujiku wakiwapokea rasmi wanafunzi Mary Bujiku na Edward Mugyabuso kwa niaba ya wahitimu wa kidato cha sita kwenda kuwalea kiroho.
Mkuu wa Shule ya sekondari St. Anthony Bro. Ismail Edward akisoma risala kwenye mahafali ya 20 ya kidato cha sita ambapo amewasihi wanafunzi wanaohitimu waendelee kutunza kumbukumbu ya shule hiyo na kuwa mabalozi wazuri wa St. Anthony kwa kuwa wazalendo wa kweli waliotayari kulijenga na kulilinda taifa letu na kukabiliana na changamoto za dunia ya leo hususani gonjwa hatari la Ukimwi na matatizo mengine yanayoikumba Tanzania.
Meza kuu ipitia risala ya Mkuu wa shule hiyo.
Picha juu na chini Mgeni rasmi Mstahi Meya Jerry Silaa akizungumza wakati wa mahafali ya 20 ya kidato cha sita ya St. Anthony ambapo ametoa pongezi kwa walimu na wanafunzi wa shule hiyo na kuongeza kuwa kwa sisi Watanzania Elimu ni nyenzo muhimu sana hasa katika mbio zetu za kupambana na maadui watatu; ujinga, maradhi na umaskini ambayo ni Silaha pekee ya kuwashinda maadui hao wote watatu.
Sehemu ya wahitimu wa kidato cha sita wakimsikiliza mgeni rasmi Mstahiki Meya Jerry Silaa.
Wahitimu wa kidato cha sita wakielekea kukabidhi zawadi kwa mgeni rasmi Mstahiki Meya.
Mgeni rasmi akifingua zawadi hiyo mbele ya wahitimu hao.
Mstahiki Meya Jerry Silaa akionyesha zawadi aliyokabidhiwa na wahitimu wa kidato cha sita ambapo walimtaka kuiweka ofisini kwake ili aendelee kuwakumbuka.
Picha Juu na Chini Mgeni rasmi Mstahiki Meya Jerry Silaa akikabidhi vyeti na zawadi kwa wahitimu wa kidato cha sita wa St. Anthony katika sherehe za mahafali ya 20 shuleni hapo.
Mstahi Meya Jerry Silaa akishow love na mmoja wa wanafunzi wanaohitimu aliyesoma kombi kama aliyosoma Mstahiki.
Mhitimu wa Kidato cha Sita Yvonne Laurent Mganga akipongezwa na familia yake baada ya kuhitimu kidato cha Sita.
Mgeni rasmi Mstahiki Meya Jerry Silaa (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya St. Anthony Bi. Fides Challe (wa tatu kushoto waliokaa), wageni waalikwa pamoja na uongozi wa shule hiyo.
Mgeni rasmi Mstahiki Meya katika picha ya pamoja na wajumbe wa kamati ya burudani wa shuleni hapo.