RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Jaji Aloysius Kibuuka Mujulizi, kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania. Taarifa iliyotolewa leo, Jumanne, 12 Februari, 2013 mjini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) Balozi Ombeni Y. Sefue, inasema kuwa uteuzi huo ulianza Februari 8, mwaka huu, 2013. Kabla ya uteuzi huu, Jaji Mujulizi alikuwa Mkuu wa Chuo cha Sheria, Lushoto.