Miss Utalii Tanzania 2012/13 Kutembelea Hifadhi za Taifa

Washiriki wa miss utalii


Miss Utalii Tanzania 2012/13 wiki ijayo wataanza ziara ndefu ya kutembelea Hifadhi za Taifa na vivutio vya utalii katika mikoa ya Dar es salaam, Morogoro, Mtwara, Lindi na Pwani. Miongoni mwa vivutio hivyo ni pamoja na Hifadhi za Taifa za Mikumi, Udizungwa, Saadani, Selous, pia maeneo ya kihistoria ya Bagamoyo, Amboni, Kijiji cha makumbusho,Makumbusho ya Taifa, Pugu sekondari, maeneo mengine ni ufukwe wa kigamboni, soko la kimataifa la magogoni.
Vivutio vingine vitakavyo tembelewa ni pamoja na uwanja wa taifa, J.K.Nyerere Air Port, Soko la kariakoo, mashule ya sekondari na msingi, pia watatembelea manispaa za ilala, temeke na kinondoni ambapo watakutana na viongozi wakuu wa wilaya, mikoa, na wabunge katika majimbo ya mikoa hiyo.