Matukio mbalimbali bungeni, Dodoma

Mbunge wa Jimbo la Mtera Livingstone Lusinde akichangia bajeti ya serikali ya mwaka 2011/2012 iliyowasilishwa hivi karibuni na Waziri wa Fedha na Uchumi Mustapha Mkulo na kuhoji uchelewaji wa baadhi ya ofisi za serikali na Viongozi mbalimbali kuhamia mjini Dodoma ambako ndio makao makuu ya nchi leo mjini Dodoma.

Mbunge wa Vunjo na Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa Augustino Mrema akiingia ndani ya ukumbi wa Bunge kuhudhuria kikao cha nane cha Bunge leo mjini Dodoma. Picha na Aron Msigwa.