Meya wa Ilala Awataka Watanzania Kuona Suala la Usafi linamgusa Kila Mmoja

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa (wa kwanza kushoto) akiongoza umati wa wafanyakazi wa kampuni ya Green Waste Pro ltd, wadau wa mazingira, maafisa wa manispaa ya Ilala na wakazi wa kata ya Kisutu wakati wa zoezi la kufanya usafi wa mazingira lilioendeshwa na kampuni ya Green Waste Pro ltd katika maeneo ya kata hiyo ikiwemo mitaro, barabara na maeneo ya wazi na kwingineko.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akizungumzia mwamko wa watanzania katika kujitolea kufanya usafi ambapo amesema, bado ni mdogo ndio maana tulisema wakati ule tunaanza mwezi wa saba tutumie karibu miezi mitatu tutoe elimu, lakini tumeongeza miezi mitatu mpaka Desemba na tukaongeza miezi mingine mitatu mpaka Machi, tutoe elimu ili ifike wakati watu wote waone ni majukumu yao kuhakikisha mji uko safi.

Amesema kuwa wamefanya kampeni hii Usafi kuanzia Kata ya Kivukoni na leo Kata ya Kisutu na wiki ijayo wanatarajia kuwa Kata ya Mchafukoge.

Ameongeza kuwa sasa tumeona iko haja ya kuanza kutekeleza sheria, hivyo tunafanya kampeni hizi tukiwa na askari wetu wa jiji na pale tutakapoona mtu au sehemu inatuchafulia mazingira kwa makusudi basi askari watatumika. Mstahiki Meya amesema anaamini kama kila mtu anaweza kuoga mwili wake, kusafisha nyumba yake basi anaweza kuyaweka safi mazingira yanayo mzunguka.

 

Meneja Msaidizi wa Kampuni ya Usafi ya Green Waste Pro ltd Bw. Abdallah Mbena akizungumzia kampeni hizo za usafi amesema zilianza tangu tarehe 19 Januari katika Kata ya Kivukoni ambapo watu wamejitokeza kwa wingi sana na kufanikiwa kutoa taka nyingi sana katika maeneo ya ufukweni.

Amesema ni kitendo cha kushukuru kuwa watu sasa hivi wanaelewa na kuanza kushiriki katika suala zima la mazingira na pia kuna viongozi wengi wameacha shughuli zao wakaja kushiriki katika kampeni hii ya usafi hivyo zoezi hili likitoka hapa litahamia Kata ya Mchafukoge.

Baada ya kuhitimisha zoezi hilo katika kata hizo tunataka liwe zoezi endelevu, hatutaki liwe la nguvu za soda kama wengine wengi wameanzisha mikakati kama hii baadae wameishia kwenye makapu, sisi tutaanzisha vipindi katika Television lakini pia katika tarehe za katikati hapa tumeanzisha program ya elimu mashuleni

Amesema wameanza na shule ya Bunge ambapo amesema katika hatua inayofuata watafanya program na wanafunzi kwa lengo la kusambaza elimu miongoni mwa wanafunzi.

 


Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa (wa kwanza kushoto) akiongoza umati wa wafanyakazi wa kampuni ya Green Waste Pro ltd, wadau wa mazingira, maafisa wa manispaa ya Ilala na wakazi wa kata ya Kisutu wakati wa zoezi la kufanya usafi wa mazingira lilioendeshwa na kampuni ya Green Waste Pro ltd katika maeneo ya kata hiyo ikiwemo mitaro, barabara na maeneo ya wazi na kwingineko.

Afisa Habari wa kampuni ya usafi ya Green Waste Pro ltd Vidah Fammie (wa kwanza kushoto) akishiriki zoezi hilo.

Umoja ni Nguvu Utengano ni Dhaifu………zoezi la kufagia barabara zinazoizunguka kata ya Kisutu likiendelea.

Moja ya magari ya kisasa ya kampuni ya Green Waste Pro ltd likifagia barabara kwa kutumia Teknolojia inayoenda na wakati.

Barabara ya mzunguko wa DTV ikifagiliwa.

Vijana wakichapa kazi.

Mstahiki Meya Jerry Silaa akimkemea mmoja wa wafanyabiashara ya Chai pembezoni mwa barabara karibu na maeneo ya DTV anayeosha vyombo na kumwaga maji yenye uchafu barabarani.

Mstahiki Meya Jerry Silaa akimuonya kuacha tabia hiyo na kumtaka kufuata utaratibu wa kutunza mazingira kama unavyoelekezwa na manispaa ya Ilala na Kampuni ya usafi ya Green Waste Pro ltd.

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Green Waste Pro Ltd. Bw. Anthony Mark Shayo akiunga mkono zoezi la usafi katika maeneo ya Kata ya Kisutu Uhindini jijini Dar leo.

 


Mstahiki Meya Jerry Silaa na viongozi wa manispaa ya Ilala wakifagia korido za majengo ya maeneo mbalimbali ya Kisutu.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akiwashukuru wafanyakazi wa kampuni ya usafi katika manispaa ya Ilala ya Green Waste Pro ltd pamoja na wakazi wa kata ya Kisutu waliojitokeza kufanikisha zoezi la usafi katika mazingira yanayowazunguka na kuwataka kujenga utamaduni wa kutunza mazingira.