JK Akutana, Afanya Mazungumzo na Maafisa Waandamizi wa Serikali za Burundi na DRC

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete Jumapili, Februari 3, 2013, amekutana na kufanya mazungumzo na maofisa waandamizi wa Serikali za nchi jirani za Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).
Katika mikutano miwili tofauti, Rais Kikwete amekuta na nakuzungumza na Mwenyekiti wa cha matawala cha Burundi cha CNDD-FDD, Paschal Nyabenda ambaye pia ni Seneta wa Jimbo la Makamba na pia amekutana na Katibu Mkuu wa cha matawala cha PPRD cha DR-Congo Bashab Evariste katika mazungumzo yaliyofanyika Ikulu Ndogo mjini Kigoma ambako Rais Kikwete yuko kwenye ziara ya siku tatu ya kikazi Mkoani Kigoma.
Nyibenda na Evariste wako nchini kwa mwaliko wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kuhuduria Sherehe za Miaka 36 yaKuzaliwa kwa chama hicho. Katika mazungumzo na Nyabenda yaliyo hudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) naKatibuwa Mambo yaNjenaUshirikianowaKimataifawa Chama hicho, Asha Rose Migiro,viongozi hao wawili walijadili masuala yanayohusu uhusiano katiya Tanzania na Burundi likiwamosuala la wakimbiziwa Burundi ambaowamepewauraiawa Tanzania.
Rais Kikwete na Nyabenda pia wamezungumzia jinsi gani Tanzania inavyoweza kutoa ardhi ya kupanua kiwanda cha sukari kilichoko mpakani mwa Tanzania na Burundi. Kiwanda hicho kiko katika Burundi lakini eneo kubwa zaidi la kulima miwa likoupandewa Tanzania kwenye Bonde la Mto Malagarasi mpaka ni mwa nchi hizo mbili.
Rais Kikwete amekishukuru CNND-FDD kwakukubali mwaliko wa CCM kushiriki sherehe hizo wakati Nyibenda ameishukuru Tanzania kwa mchango wake wa miaka mingi katika kutafuta suluhu ya vita vya wenyewe kwa wenyewe katika Burundi.
Katika mazungumzo yake na Evariste, Rais Kikwete amemjulisha mjumbe huyo kutoka DRC kuhusu juhudi zinazofanywa na nchi za ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Afrika katika kutafuta amani na utulivu katika eneo la mashariki mwa DRC ambako kundi la waasi la M23 linapigana majeshiya Serikali ya Rais Joseph Kabila.
“Sisi Tanzania tukotayari kuchangia batalioni moja kwenye Jeshi la Kimataifa Lisiloegemea Upande Wowote(INF). Huu ndio mchango ambao tunaweza kutoa kwa ndugu zetu, majirani zetu na marafiki zetu,” amesemaRaisKikwete.