Waziri wa Habari na Utamaduni Atembelewa na Makamu Meya wa Manispaa ya Tianjin

Makamu Meya wa Manispaa ya Tianjin kutoka China Bi. Zhang Junfang, (wa pili kulia) akikabidhi picha ya kiutamaduni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk.Fenella Mukangara wakati apomtembelea leo ofisi kwake jijini Dares Salaam, ikiwa ni ishara ya ushirikiano wa kiutamaduni baina ya nchi yake na Tanzania.Meya huyo yuko nchini kwa ajili ya sherehe za mwaka wa Kichina zitakazoadhimishwa jioni kwenye uwanja wa Mnazimmoja, Dar es Salaam. Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda.

Makamu Meya wa Manispaa ya Tianjin kutoka China Bi. Zhang Junfang, (wa pili kulia) akifafanua kuhusu ushirikiano wa kiutamaduni baina ya nchi yake na Tanzania kwa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk.Fenella Mukangara wakati apomtembelea leo ofisi kwake jijini Dares Salaam. Meya huyo yuko nchini kwa ajili ya sherehe za mwaka wa Kichina zitakazoadhimishwa leo jioni kwenye uwanja wa Mnazimmoja, Dar es Salaam. Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda.

WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda leo jioni anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya sherehe za mwaka wa Kichina zitakazofanywa kwenye uwanja wa Mnazimoja, jijini Dar es Salaam.
Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk.Fenella wakati Makamu Meya wa Manispaa ya Tianjin kutoka China Bi. Zhang Junfang, alipomtembelea ofisini kwake kwa lengo la kuzungumzia ushirikiano wa kiutamaduni baina ya nchi hizo mbili.
Aidha Waziri huyo aliwataka Watanzania kujitokeza kwa wingi na kutumia nafasi hiyo kuweza kujifunza utamaduni baina ya nchi hizo mbili.
“Watanzania wajitokeze ili kjifunza utamaduni mbalimbali kati ya nchi hizi. Katika sherehe hizo kutakuwa na kikundi cha utamaduni kitaonyesha michezo ya sarakasi, kareti na kuigiza. Pia kutakuwa na kikundi cha sanaa kutoka TaSuBa,” alisema.
Aliwataka wachongaji vinyago kutumia fursa hiyo ili kuweza kuboresha bidhaa wanazozitengeneza.
Waziri huyo aliishukuru nchi hiyo kwa misaada ya vifaa mbalimbali vya ofisi iliyotoa kwa wizara yake. Hata hivyo alisema sekta hiyo iinakabiliwa na changamoto za ukosefu wa waatalamu wa utamduni na miundombinu yake.
Kwa upande wake Bi. Zhang Junfang, aliishukuru nchi ya Tanzania kwa ukarimu na kuonyesha ushirikiano wa kiutamaduni.