Rais Jakaya Atuma Salama za Rambirambi kwa KKKT

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Kiongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Askofu Mkuu Dkt. Alex Malasusa kuomboleza kifo cha Mchungaji Mstaafu wa Kanisa hilo, Mzee Thomas Mussa, aliyepata pia kuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM).
Katika salamu zake alizozituma Februari 2, 2013, Rais Kikwete amemwambia Askofu Mkuu Malasusa kuwa amesikitishwa na kuhuzunishwa na taarifa za kifo cha Mzee Thmoas Mussa kilichotokea, Februari Mosi, 2013, katika Hospitali ya Mkoa wa Singida alikokuwa amelazwa.
Amesema Rais Kikwete: “TutamkumbukaMzee Thomas Mussakwamchango wake mkubwa na uongozi wake bora ndani ya Kanisa la KKKT nandaniya Chama cha Mapinduzi ambako alikuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa. Alitoa uongozi wa kiroho na uongozi wa kisiasa kwauwiano na kwa namna ambayo itaendelea kuwa mfano wa kuigwa”
“Nakutumiawewe Baba AskofuMkuu Alex Malasusa salamu zangu za rambirambi na kupitia kwako pia na tuma salamu za pole nyingi kwa viongozi wenzako na waumini wa Kanisa la KKKT ambao wamempoteza kiongozi na mwumini mwenzao,” amesema Rais Kikwete na kuongeza:
“Aidha, kupitia kwako Baba AskofuMkuu, naitumiafamiliayaMzee Thomas Mussa salamu za rambirambi za dhati ya moyo wangu kwa kuondokewa na baba, babu na mhimili wa familia. Wajulishe kuwa nikonao katika kipindi hiki kigumu na naungana nao kuomboleza. Aidha, naungana nao katika kumwomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, aiweke peponi pema roho ya Marehemu Askofu Thomas Mussa. Amen.”