Na muandishi wetu, Santa Barbara, California.
Wimbi la ombaomba limekuwa ni kero kwa wakazi na watalii wa mji wa Santa Barbara hapa USA. Uchunguzi uliofanyika na dev.kisakuzi.com umebaini kwamba kuna vijana wengi wapo mtaani wanazagaa bila kazi.
Wengi wa vijana hao imebainika wana matatizo ya akili, na baadhi yao wameamua tu kuelekeza nguvu zao kwenye biashara hiyo ya kuomba, ambayo wanadai inalipa zaidi ukizingatia mji wa Santa Barbara una matajiri wengi wenye huruma.
Mmoja wa ombaomba hao alinaswa na thehabari akiwa na bango lenye ubunifu mkubwa wa maneno yasemayo “I’m like Obama, I want change”, akimaanisha kwamba “Mimi ni kama Obama, nataka mabadiliko”(kwa maana nyingine anataka pesa).
Tatizo la ombaomba halipo Tanzania tu peke yake, isipokuwa tofauti kubwa iliyopo ni kwamba wenzetu Wamarekani wamejipanga na mapogramu mbalimbali ya kusaidia watu hawa, na wale ambao wapo tayari basi msaada upo. Je serikali yetu ya Tanzania ina mkakati wowote wa kusaidia ombaomba hapo nyumbani?
Hapo juu ni picha tofauti za ombaomba hao wakiwa kazini na pia wakiwa mapumzikoni.
Picha zote na Mpiga Picha maalum wa dev.kisakuzi.com, Santa Barbara