MAWAZIRI waliokuwa kikaoni ni pamoja na Waziri wa Ujenzi (Dkt. John P. Magufuli), Waziri wa Uchukuzi (Dkt. Harrison Mwakyembe), Waziri wa Viwanda na Biashara (Abdallah Kigoda), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwezeshaji na Uwekezaji, – (Dkt. Mary Nagu) na Waziri wa Elimu (Dkt. Shukuru Kawambwa).
2· Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mjini, Wilman Kapenjama Ndile alitamka kuwa Waandishi wa habari wamealikwa kwa ajili ya kikao cha muhstasari (briefing) wa “Yatokanayo”.
3· Katibu Mkuu wa Shura ya Maimamu kwa Mkoa wa Mtwara, Sheikh Idrissa Lingondo amesema kilichosabababisha vurugu na yote ya uharibifu yaliyotokea katika kipindi hiki, ni kauli mbovu za kuudhi na kuvunja moyo kama vile kukataa kupokea maandamano ya watu na kuwaita wahaini na/au wapuuzi. Majibu kama hayo ndiyo yaliyoamsha hasira.
Akashauri kuwa watu wote (viongozi kwa wananchi) watumie diplomasia. Akatoa wito kwa Wananchi kuwa wasikivu na watulivu katika kipindi hiki ambacho mazungumzo na Viongozi wa juu wa Serikali yanaendelea.
4· Askofu George Mussa wa Kanisa la TAG (Tanzania Assemblies of God), alisema ukimya wa viongozi na kutokukubali kuzungumza na wananchi na kuwajibu maswali yao, ndiyo uliochochea wananchi kushikwa na hasira iliyosababisha hasara. Akahoji ni kwa nini viongozi wanakuwa kimya kusubiri mpaka maafa yanapotokea ndipo wanajongea kuzungumz a na Wananchi?
Akasisitiza kuwa siyo kwa Mtwara tu, bali nchi nzima, kwamba wananchi wamekuwa wanapuuzwa na hawasikilizwi hoja zao hasa pale wanapotaka kuwasilisha masuala yanayowazunguka. Akaonya kuwa maandiko ya Biblia yanasema Waisraeli waliopacha kusikiliza kilio cha watu wao, Mungu aliruhusu uasi utendeke, ndipo Watawala walipoamka na kuwasikiliza.
Askofu Mussa akasema kuwa mtu yeyote ana haki, hata kama hajaenda shule, kwani hilo halimaanishi kuwa hajui kuhusu yanayomzunguka. Akasema iachwe dharau ya kudhani kuwa Watu wa Kusini hawajasoma au/wala kuelimika.
Amehoji, ikiwa ahadi walizopewa wananchi –kujenga mitambo ya miradi, kutoa ajira n.k.– haijawekwa wazi, Je, Wananchi wataijuaje? Ni wazi kuwa watahoji.
Alipotakiwa kutoa maoni yake kwa ujumla, alionya dhidi ya matumizi ya nguvu kwa kusema kuwa mara nyingi nguvu za Watawala huzaa uasi wa Wananchi ili kukabiliana na nguvu hizo, akasema ndiyo mifano iliyotokea kwenye nchi ambazo zimejitahidi kutumia mabavu kuongoza wananchi.
Kuhusu nafasi yao kama viongozi kushirikishwa katika masuala ya kijamii, ameuliza, vioangozi wanasubiri mpaka machafuko yatokee ndipo maombe viongozi wa dini wawatulize wananchi?
Mwishowe akaomba na kuwasisitiza Wananchi wawe watulivu, wasikivu, Waitii mamlaka –kama agizo la Mungu katika Biblia linavyosema– na kutokuasi kwani ni laana kwa Taifa.
– Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Mstaafu Simbakalia kawaomba radhi wananchi wa Mtwara.
– Waziri Nchimbi kutumia lugha kibabe na vitisho dhidi ya raia pamoja na taarifa isiyokuwa na tathmini halisi na yenye uwiano pale alipotolea mfano askari aliyevamiwa dukani/baa yake na kuibiwa pesa kiasi cha sh. 1,895,000/= na kupoteza mali ya sh. 200,000,000/= (milioni mia mbili) na kusababisha watu wagune.
– Kawambwa kawahimiza wazazi kuwaruhusu watoto kwenda shule kupata elimu sanjari na chuo cha VETA kutoa masomo ya mitaala ya gesi sanjari na uchomeleaji baharini.
– Tibaijuka amezungumzia kuhusu upanuzi wa mji wa Mtwara na kuleata kauli mbiu ya “Amani na Maendeleo” kutoka kwao Kagera.
– Mwakyembe amezungumzia upanuzi wa bandari kavu na ujenzi wa reli Mtwara, Liganga, Mchuchuma hadi Mbamba Bay na kuahidi kuja Mtwara kila baada ya miezi 3 na kujadili na kutathmini changamoto.
– Waziri Mkuu ametoa udhuru wa Waziri wa ujenzi Dk Magufuli ambaye alitakiwa kuwepo lakini hakuweza kuhudhuria.
– Bi Mapunjo kaahidi mipango mikubwa ya ujenzi wa viwanda mkoani Mtwara.
– Mbilinyi kaainisha idadi ya makampuni yaliyoonyesha nia ya kuja kuwekeza Mtwara (sina hakika sana kama ni Mtwara).
– Waziri Mkuu katoa majumuisho ya ziara yake ambayo hayana tofauti na haya yaliyojadiliwa.
CHANZO: www.wavuti.com na Kumekucha Blog (Mtwara)