Kutoka kulia ni Rodney Rugambo, Wawila Nzowa, Evelyne Auguste na Dennis Rauya wakifuatilia maelezo ya mmoja wa wataalam wa mtandao huo wakati wa uzinduzi huo.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria katika uzinduzi wa mtandao huo.
Ofisa Masoko wa Benki ya ABC Evelyne Auguste akitoa maelezo juu ya udhamini wa benki hiyo kwa mtandao wa Ligikuu.
Rodney Rugambo Meneja Masoko wa Push Mobile akizungumzia udhamini wa kampuni hiyo kwa mtandao huo ili kuboresha mchezo wa miguu hapa nchini .
Meneja Mawasiliano wa Vodacom Salim Mwalim akiishukuru kampuni hiyo kwa kuanzisha mtandao huo ambao amesema utasaidia sana kutangaza mpira wa miguu nje ya nchi na kuwatangaza wachezaji wa Ligi Kuu ya Vodacom.