Golikipa wa timu ya Black Leopards, Posnett Omony akisota kuokoa mpira uliotinga wavuni kutoka kwa mchezaji wa timu ya Yanga, Jerry Tegete kwa njia ya penati mnamo dakika ya 54. Timu ya Yanga imeibuka kifua mbele mpaka dakika 90kwa kuinyuka goli 2-1 timu ya Black Leopards kwenye mchezo wao wa marudiano wa kirafiki uliofanyika kwenye uwanja wa CCM-Kirumba jijini Mwanza.
Wachezaji wa timu Yanga wakifurahia goli la pili lililofungwa na Jerry Tegete kipindi cha pili mnamo dakika ya 54 kwa njia ya penati.
Mchezaji Hamis Kiza wa Yanga akifanya jitihada za kumchomoka beki wa timu ya Black Leopards, Victor Kamhuka.
Mchezaji wa wa timu ya Yanga David Luhende akitaka kumchomoka mchezaji wa timu ya Black Leopards, Moses Kwena, kwenye mchezo wao wa marudio uliofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Baadhi ya mashabiki wa Mpira wakiwa wamepanga mstari kwa ajili ya kununu tiketi na kujionea kandanda safi kabisa kati ya timu ya Yanga na Black Leopards ya Afrika kusini.
Kikosi cha Yanga kikiwa katika picha ya pamoja.
Sehemu ya umati wa watu waliokuwa wakishuhudia mchezo huo, ambapo timu ya Yanga imetoka kifua mbele goli 2-1 dhidi ya timu ya Black Leopards ya Afrika Kusini, mchezo huo umechezwa leo kwenye uwanja wa CCM-Kirumba jijini Mwanza.
Mtanange ukikaribia kuanza.
Kikosi cha timu ya Black Leopards.
Benchi la ufundi la timu ya Yanga
Ilikuwa ni patashika ngua kuchanika, mchezaji wa timu ya Yanga, Jerry Tegete akiwatoka baadhi ya mabeki wa timu ya Black Leopards, Jerry alifanikiwa kufunga goli la pili mnamo dakika ya 54 kipindi cha pili.
Nginja nginja tuu
Makocha wakipongezana mara baada ya mpira kuisha.
Sehemu ya Umati wa mashabiki wa timu ya Yanga.