KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na mgeni wake, Balozi wa Uingereza hapa nchini, Diane Corner, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo Januari 22, 2013. Kushoto ni Katibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro na kulia ni Mkuu wa Mawasiliano na Siasa wa Ubalozi huo, Mark Polatajko.
KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiagana na Balozi wa Uingereza hapa nchini, Diane Corner, baada ya mazungumzo yao, leo, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo Januari 22, 2013. Wapili kulia ni Katibu wa NEC ya CCM, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro na kulia ni Mkuu wa Mawasiliano na Siasa wa Ubalozi huo, Mark Polatajko. (Picha na Bashir Nkoromo).