Dk Bilal Ahudhuria Mazishi ya Makamu wa Rais Zimbabwe

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiweka shada la maua kwenye kaburi la Makamu wa Rais wa Zimbabwe Marehemu Dk. Landa John Nkomo wakati wa mazishi yake yaliyofanyika jana kwenye Makaburi ya Mashujaa jijini Harare. (Picha na OMR)


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal kushoto akizungumza na Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe alipomtembelea Ikulu ya Harare jana kwa lengo la kumfariji kutokana na kifo cha Makamu wa Rais wa nchi hiyo Marehemu Dk. Landa John Nkoma kilichotokea mwanzoni mwa wiki iliyopita na kuzikwa jana katika Makaburi ya Mashujaa jijini Harare. Katikati ni Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe Adadi Rajabu.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal akifurahia jambo na Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe kwenye Ikulu ya nchi hiyo jijini Harare baada ya kumaliza mazungumzo yao. Makamu wa Rais alimtembelea Rais Mugabe kwa lengo la kumfariji kutokana na kifo cha Makamu wake Marehemu Dk. Landa John Nkomo kilichotokea mwanzoni mwa wiki iliyopita. Dk. Nkomo alizikwa jana kwenye Makaburi ya Mashujaa jijini Harare.