Uchaguzi Tanzania Premier League Board (TPL)

Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah

Uchaguzi Tanzania Premier League Board (TPL)

1. Kamati ya Uchaguzi ya TFF imepitia Fomu za waombaji uongozi wa TPL Board na kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi za TFF ibara ya 11(1), (2) na (3), waombaji uongozi wafuatao majina yao na nafasi wanazoomba kugombea yanawekwa wazi kutoa fursa kwa wale wote wenye pingamizi kwa nini mwombaji aliyetajwa hapa chini asiteuliwe kugombea nafasi aliyoomba, wawasilishe pingamizi zao kwa Katibu Mkuu wa TFF, kuanzia tarehe 22 Januari 2013 hadi tarehe 26 Januari 2013 saa 10.00 jioni.

2. Pingamizi sharti liwe kwa maandishi, lieleze kwa uwazi sababu za pingamizi, liambatanishwe na ushahidi wa pingamizi, liwe na jina kamili la mtoa pingamizi, anwani ya kudumu na saini yake.

NAFASI INAYOGOMBEWA S/No. JINA

MWENYEKITI WA TPL BOARD
1. Hamad Yahya Juma
2. Yusufali Manji

MAKAMU MWENYEKITI WA TPL BOARD 1. Said Mohamed

MJUMBE –KAMATI YA UENDESHAJI (Management Committee) 1. Christopher Peter Lukombe
2. Kazimoto Miraji Muzo
3. Omary Khatibu Mwindadi

Kamati ya Uchaguzi
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania