Ziara ya dev.kisakuzi.com Nchini Kenya -2

Moja ya mabango makubwa ambayo yameenezwa pembezoni mwa barabara za Kenya na wanasiasa kujinadi


HIVI sasa unapopicha maeneo anuai ya majiji ya Mombasa na Nairobi utakutana na mabango ya wagombea wa vyama mbalimbali vya siasa wakijitangaza kwa wapiga kura pamoja na kauli mbiu zao kujinadi kwa Wakenya. Mabango mengi makubwa na ya kuvutia yamewekwa pembezoni mwa barabara ili yaonekane vema.

Mabango haya ni ya thamani na gharama kubwa ambayo kwa nchi kama Tanzania yanatumiwa na makampuni makubwa ya biashara kutokana na gharama yake kimalipo. Kwa Kenya wagombea wenyewe wanaweza kumudu gharama hizo za matangazo, wagombea wengi ni wafanyabiashara wakubwa na watu wenye fedha ambao suala la fedha si tatizo kwao.

“Huku wagombea wengi ni wafanyabiashara wanafedha nyingi hivyo wanaweza kugharamia kabisa matangazo kama hayo (mabango makubwa) kwao hilo si tatizo…wapo baadhi ya wagombea wanamiliki hadi helkopta hawa ni watu wenye fedha,” anasema mmoja wa wananchi wa Kenya alipokuwa akizungumza na dev.kisakuzi.com nchini Kenya.

Makundi na mikusanyiko mbalimbali nchini Kenya kwa sasa yanajadili uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Kenya mwezi Machi, 2013. Kampeni zina pamba moto ikiwa mirengo itakayochuana katika kinyang’anyiro cha Uchaguzi Mkuu ni ule unaoundwa na Naibu Waziri Mkuu wa Kenya Uhuru Kenyatta na hasimu wake wa zamani William Ruto ambao wote wana kesi katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) wakihusishwa na machafuko ya baada ya uchaguzi wa Disemba 27, 2007.

Muungano mwingine ni ule wa Waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga na Makamu wa Rais Kalonzo Musyoka huku watatu ukiundwa na wabunge, Rafael Tuju na Peter Keneth, Waziri wa Sheria, Eugine Wamalwa na Naibu Waziri Mkuu Musalia Mudavadi muungano ambao wachambuzi wa mambo wanaamini ni wa watu safi na wachapakazi.

Zifuatazo ni picha mbalimbali zilizopigwa katika ziara hiyo nchini Kenya

Baadhi ya mabango makubwa nchini Kenya yalioenea katika barabara tofauti kuwanadi wagombea. Habari zaidi za ziara hiyo zinakujia, fuatilia mtandao huu