Kijue Kipindi cha ‘Mimi na Tanzania’

Kijue Kipindi cha ‘Mimi na Tanzania’

MIMI na Tanzania‚ ni kipindi kinachohusu masuala yanayoigusa jamii kwa namna moja au nyingine haswa katika siasa, uchumi,michezo,na vikwazo na vimbwangwa vinavyoikumba jamii ya kitanzania.

Mimi Na Tanzania ni kipindi kisicho na upendeleo katika kumsaidia mwananchi wa kawaida haswa unyanyasaji unaofanywa na wanaodhani wana nguvu kuliko aliyewaumba.

Tunamulika Kaskazini hadi Kusini, Magharibi hadi mashariki ili kujenga jamii yenye amani, haki na upendo.

Mimi Na Tanzania ni kipindi pekee kinachofunga safari kutafuta habari za kijamii popote pale Tanzania.

Usikose kutazama kipindi hiki kila siku ya Jumapili Saa moja na nusu jioni katika kituo cha Televisheni cha Channel Ten.

Kipindi cha ‘Mimi na Tanzania’ kinaongozwa na mrembo aliyewahi kushika taji Miss Tanzania mwaka 1999 Hoyce Temu.

Pia unaweza kupata vipindi vipya vinavyoigusa jamii kwa kuetembelea libeneke lake hapa http://www.miminatanzania.co.tz/ Unaweza pia kulike page kwenye mtandao wa facebook humu http://www.facebook.com/miminatanzania

Fuatilia moja ya kipindi cha madhara ya madawa ya kulevya hapo chini.