Mwenyekiti AU Kufanya Ziara Tanzania

Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) na Rais wa Benin, Boni Yayi

Na Mwandishi Wetu

Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) na Rais wa Benin, Boni Yayi anawasili nchini usiku wa leo (Januari 15, 2013) kwa ziara ya kikazi ya siku mbili katika Tanzania.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo kwa vyombo vya habari na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu; mara Yayi atakapowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere mjini Dar es Salaam, atapokelewa na Mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete.

Baadaye usiku, viongozi hao wawili watafanya mazungumzo kuhusu masuala mbali mbali yanayolihusu Bara la Afrika kabla ya kiongozi huyo wa Benin kuondoka nchini asubuhi ya Januari 16, 2013.