RAIS wa zamani wa Misri, Hosni Mubarak, ameruhusiwa kufanyiwa kesi nyengine kwa makosa ya kutozuwia mauaji ya waandamanaji mamia kadha wakati wa ghasia zilizomuondoa madarakani. Mahakama ya rufaa mjini Cairo, baada ya kikao kifupi, yalitoa amri hiyo ya Bwana Mubarak kufanyiwa kesi nyengine.
Mwezi wa Juni mahakama yalitoa hukumu ya kifungo cha maisha kwa Rais Mubarak kwa hatia ya kuwa na dhamana ya mauaji ya waandamanaji yaliyofanywa na askari wa usalama ambao wakijaribu kuzima ghasia za mwaka wa 2011.
Mkuu wa usalama wa Bwana Mubarak, Habib el-Adly, ambaye anatumika kifungo cha maisha kwa mashtaka kama hayo, piya atafanyiwa kesi nyengine.
-BBC