TIMU ya AZAM FC imefanikiwa kutwaa Kombe la Mapinduzi ya Zanzibar baada ya kuifunga timu ya Tusker ya Kenya mabao 2-1. Tusker ndiyo ilikuwa ya kwanza kuifunga timu ya Azam kabla ya timu hiyo kugeuka na kusawazisha kwa penati na kuongeza bao la ushindi.
Azam FC ambayo imecheza ikiwa na idadi kubwa ya wachezaji wake majeruhi na wengine wakiwa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imefanikiwa kutwaa kombe hilo kwa mara ya pili mfululizo baada ya mwaka jana tena kulitwaa mjini Zanzibar.
Hata hivyo Kocha wa Tusker alionekana kulalamika baada ya mchezo huo kumalizika akidai waamuzi wamemuangusha kwani walikuwa wakiipendelea Azam FC jambo ambalo alidai limechangia kumnyima ushindi. Akizungumzia hali ya mchezo alisema Azam ni timu nzuri lakini inapaswa kujiandaa zaidi, na kuacha kutegemea baati za kupendelewa. Aliongeza kuwa idadi kubwa ya wachezaji wake wapo timu ya taifa na wengine hawakuja katika mashindano hayo hivyo kuchangia kumuangusha kimchezo.
Kwa ushindi huo Azam FC imefanikiwa kujinyakulia kitita cha sh milioni 10 pamoja na kombe la Mapinduzi, huku Tusker ya Kenya ikijipatia Kombe la nafasi ya pili na fedha.