Taifa Stars Yawasili Salama Ethiopia, Kukipiga Leo

Baadhi ya wachezaji wa Taifa Stars

TAIFA Stars imefika salama nchini Addis Ababa tayari kwa mechi ya kirafiki dhidi ya wenyeji Ethiopia inayotarajia kufanyika leo. Mechi inachezwa Januari 11 Addis Ababa Stadium kuanzia saa 11.30 jioni( Tanzania na Ethiopia hatupishani saa). Timu imefikia Hilton Hotel. Ilifanya mazoezi jana jioni Addis Ababa Stadium kwa saa moja kuanzia saa 11.30 jioni.

Boniface Wambura, Ofisa Habari
Tanzania Football Federation