Asante Modern Coast kwa kuisafirisha dev.kisakuzi.com kuelekea Kenya. Basi la kampuni ya Modern Coast likiwa limeegesha kwenye mgahawa wa Rusharoho Mjini Tanga likisubiri abiriwa wakipata mlo wa mchana kabla ya kuendelea na safari kuelekea nchini Kenya. Mwandishi wa dev.kisakuzi.com alikuwa ni mmoja wa habiria hao.
<strong>MTANDAO</strong> wa dev.kisakuzi.com hivi karibuni ulifanya ziara nchini Kenya katika majiji ya Nairobi na Mombasa kwa kutembelea maeneo kadhaa ya majiji hayo maarufu kwa ajili ya kujifunza masuala mbalimbali ya kimaendeleo pamoja na kubadilishana matukio hasa kipindi hiki ambapo nchi ya Kenya inaendelea kujiandaa na uchaguzi mkuu. Zifuatazo ni picha anuai ambazo dev.kisakuzi.com ilizipiga kwa ajili ya matukio yaliojiri katika ziara hiyo.
Geti la mpaka wa Kenya na Tanzania eneo la Horohoro mjini Tanga. Eneo hili abiria hushuka na kugoga pasi za kusafiria pamoja na kugaguliwa kabla ya kuvuka.
Baada ya kuingia Jijini Mombasa utaratibu wa kusafiri uligeuka na kuanza kusafiri usiku. Nchini Kenya mabasi makubwa hufanya safari zake usiku kwa usiku ikiwa ni usafiri wa kawaida. Hapa ni Mji Mdogo wa Mtito Andei nchini Kenya majira ya saa nane za usiku ambapo mabasi usimama abiria kupata chochoche kitu.
Hapa ni katikati ya Jiji la Nairobi kwenye moja ya kipita kulia maarufu (round about), Makutano ya Mitaa ya Haile Selassie na Moi.
Haya tena hiki ni moja ya kibao cha muwekezaji (mganga wa kienyeji) anayedai anatoka nchini Tanzania.
Mapokezi ya Mhariri Mkuu wa dev.kisakuzi.com, Joachim Mushi (kushoto) akiwa na baadhi ya wenyeji Mjini Embu kilometa kadhaa kutoka Jijini Nairobi.
Mhariri Mkuu wa dev.kisakuzi.com, Joachim Mushi (kulia) akipata picha na baadhi ya wenyeji wake Mjini Embu kilometa kadhaa kutoka Jijini Nairobi.
Mhariri Mkuu wa dev.kisakuzi.com, Joachim Mushi (kushoto) akiwa na mgombea Ubunge kwa tiketi ya Muungano wa CORD Jimbo la Embu eneo la Runyenjes nchini Kenya Alex Murithi, muungano huo utumia alama ya vidole viwili kama CHADEMA nchini Tanzania. Mgombea huyu alikuwa ni mmoja wa wenyeji wa dev.kisakuzi.com.
Bango la muungano wa CORD likiwa na picha ya mgombea David Murithi. Picha zaidi za ziara hii zitakujia kaa mkao wa kula!