Lowassa Aandaa Chakula cha Mchana Monduli Kuukaribisha Mwaka 2013

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Edward Lowassa akihutubia wageni mbali mbali waliohudhulia hafla ya Chakula cha Mchana aliyoiandaa kwa ajili ya kuukaribisha Mwaka Mpya wa 2013,iliyofanyika nyumbani kwake,Monduli.

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Edward Lowassa na Mkewe Mama Regina Lowassa wakiwapungua mikono wageni waalikwa wakati wa hafla ya Chakula cha Mchana aliyoiandaa kwa ajili ya kusherehekea Mwaka Mpya wa 2013, iliyofanyika nyumbani kwake Monduli.
Mbunge wa Jimbo la Kilindi, Beatrice Shelukindo (wa pili kulia) akiambatana na Mbunge wa Jimbo la Bariadi, Andrew Chenge wakati wakiwasili kwenye hafla ya Chakula cha Mchana iliyokuwa imeandaliwa na Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Edward Lowassa kwa ajili ya kuukaribisha Mwaka Mpya wa 2013.
Wafanyabiashara maarufu jijini Arusha,Papa King na Mdau Mathias (MNEC) wakiwasili kwenye hafla hiyo.
waalikwa wakipata Chakula nyumbani kwa, Lowassa.