Full Shangwe Blog Yawashukuru Wadau Wake

John Bukuku Mkurugezni wa Fullshangweblog akiwa katika picha ya pamoja na David Milliband aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza, Mbunge wa Jimbo la South Shield na mmoja wa wamiliki wa klabu ya Sunderland ya Uingereza wakati alipotembe klabuni hapo kikazi mwezi Oktoba mwaka jana

Napenda kutoa shukurani zangu za mwaka 2013 kwa makampuni na wadau mbalimbali waliotusapoti katika kuendeleza umuvuzishaji au kurusha matukio mbalimbali yanayotokea ndani na nje ya nchi katika mtandao wetu wa kijamii www.fullshangweblog.com kwa ushirikiano wao waliotupa wakati wote katika kipindi cha miaka minne toka tuzaliwe rasmi 2008.

Sapoti hii imetupa moyo wakujituma zaidi katika kazi lakini pia imetuwezesha kugharamia baadhi ya gharama za muhimu katika utendaji wetu wa kazi za kila siku, na kutupa jeuri angalau ya kuthubutu kupata glasi ya juisi au kikombe cha kahawa wakati tukiwa katika kompyuta zetu tukimuvuzisha matukio.

Hili si jambo dogo ni jambo la kutia moyo kwani mmethamini kile tunachokifanya kwa ajili ya kuelimisha jamii, kupasha habari na kukosoa mambo yanapokwenda ndivyo sivyo, Pia tumeweza kusafiri ndani na nje ya Tanzania kwa ajili ya kukusanya matukio mbalimbali yote ni kuokana na msaada mkubwa kutoka kwenu wadau.

Naomba nitaje baadhi ya Kampuni na wadau waliotusaidia kwa namna moja au nyingine katika ushauri wa hali na mali nikianza na Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) kupitia aliyekuwa mkurugenzi wa Kampuni hiyo Richard Wells, Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Bw. Steve Ganon, Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni hiyo Ephraim Mafuru, Mkurugenzi wa Mawasiliano Nandi Mwiyombela, Meneja wa Mawasiliano Imani Lwinga, Meneja wa Bia ya Serengeti Allan Chonjo na wafanyakazi wote wa kampuni ya bia ya Serengeti.

Napenda kutoa shukurani kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa Benki ya NBC Lawrence Mafuru, Mwinda Kiula Mkuu wa Masoko na Mahusiano, Aden Kitomari Meneja wa Matangazo na Eddie Muhina Meneja Mahusiano, kwa ushirikiano waliotupa tunasema asante sana na tuko pamoja katika ushirikiano huu mzuri kwa maendeleo ya ustawi wa jamii na taifa kwa ujumla.

Shukurani pia ziende kwa Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano Benki ya NMB, Imani Kajula , Meneja Mawasiliano Josephine Kulwa na Elizabeth Ikengo kwa ushirikiano ambao tumekuwa tukipata kutoka kwa benki hiyo na wafanyakazi wote kwa ujumla tunasema asanteni sana wadau.

Natoa pia shukurani kwa Meneja Masoko wa Kampuni ya Bayport Finacial Services Ngula Cheyo na viongozi pamoja na wafanyakazi wote wa taasisi hiyo , Viongozi na wafanyakazi wote wa Mfuko wa Afya ya Jamii (NHIF) pamoja na wafanyakazi wote na Mkurugenzi wa Kampuni ya Wilna International ya Japani Willy Ngoya kwani hawa wote tunawashukuru kwa sapoti waliyotupa kwa muda wakati ambao tumekuwa tukishirikiana nao, tunasema “Asanteni sana wadau”

Shukurani za pekee zimwendee Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Montage Limited ya jijini Dar es Salaam, Teddy Mapunda kwa ushirikiano alionipa kwakweli ninajisikia furaha kufanya kazi na Mapunda, kwani amekuwa mshauri na msaada mkubwa kwa hali na mali katika kuhakikisha Mablogger tunasonga mbele katika kazi zetu za kila siku” niwape siri wakati nikihudhuria mikutano yake ya habari aliwahi kuniuliza mbona sina (Laptop) kompyuta ya mkononi na kazi zangu nazifanyia wapi” Aliniuliza Teddy.

Nilimjibu nafanyia kwenye ‘Inernet Cafe’ kutokana na majibu hayo aliguswa sana hivyo alinipa shilingi milioni moja kwa ajili ya kununulia kompyuta.

“mkutano ujao nitakaofanya uje na kompyuta hiyo” Alisistiza Mapunda.

Kwa kweli Sina cha kuilipa Familia ya Nesto Mapunda ,mkeweTeddy Mapunda kutokana na kuwa sehemu kubwa ya mafanikio ya Shughuli zangu za kuendesha Mtandao wa www.fullshangweblog.com mungu awabariki.