JESHI LA POLISI ARUSHA KATIKA KASHFA!

Kaimu Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoani Arusha Akili Mpwapwa

Na Janeth Mushi, TheHabari, Arusha
JESHI la polisi mkoa wa  Arusha limekumbwa na kashfa nzito mara baada ya kuficha majina ya watu watatu waliouawa baada ya kufanya tukio la utekaji na ujambazi kwa wafanyabiashara watano lililojitokeza juzi majira ya saa 7;00 mchana nje kidogo ya mji wa Arusha.

Utata huo uliojitokeza katika taaarifa ya tukio hilo la ujambazi iliyotolewa na Kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoani hapa,Akili Mpwapwa jan alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari  ofisini kwake.

Mpwapwa alisema kuwa watu  hao ambao wanaodhaniwa  kuwa ni majmbazi waliuwawa
na wananchi wenye hasira kali kwa mawe katika eneo la Matejoo mara baada ya kulitekeleza gari walilokuwa wakilitumia na kisha kukimbia kwa miguu.

Mpwawpa alidai  kuwa hadi sasa jeshi hilo halijaweza kuwatambua kwa majina majambazi hao,hukua akibainisha kuwa  marehemu hao wametambulika kuwa ni wahalifu na wamehusika katika vitendo mbalimbali vya uhalifu jijini hapa  huku mmoja kati yao akihusishwa katika tukio la uporaji lililotokea eneo ya maji ya chai.

Hatahivyo,mara baada ya maelezo ya Kaimu huyo,baadhi ya waandishi wa habari walitaka kujua undani wa taarifa juu ya majambazi hao,na kufika  katika chumba cha
kuhifadhia maiti katika hospitali ya mkoa ya Mt,Meru ambapo walipatiwa majina ya marehemu hao na wahudumu wa chumba hicho.

Wahusika wa chumba hicho waliwataja marehemu hao kuwa ni Obeid Erasto(30),Raphael Patrick(37) na

Florence Basil(27)  wote wakiwa ni wakazi wa mjini  Arusha huku wakidai kuwa miili ya marehemu hao ilipelekwa hapo majira ya saa 10.30 jioni
Awali akitoa taarifa hiyo kwa vyombo vya  habari,Mpwapwa alisema kuwa juzi majira ya saa 7;00 mchana katika maeneo ya Kisongo barabara ya Arusha-Babati 
majambazi hao wakiwa na  gari lenye namba za  usajili T785 ACM aina ya Toyota mark II waliwateka wafanyabiashara hao watano waliokuwa kwenye gari aina ya Hyundai  lililokuwa na namba 

T744 BMX  lolilokuwa likitokea mjini Arusha kuelekea maeneo ya Meserani kwenye mnada wa ng”ombe.
Mpwapwa alisema kuwa   majambazi hao watatu walipofika katika eneo hilo la Mesrrani  waliwateka wafanyabiashara hao na kufanikiwa kuwapora fedha  kiasi cha sh,4.2 millioni na simu mbili za mkononi ambazo thamani yake haijaweza kufahamika mara moja.

Alkili alidai kuwa baada ya kufanikiwa kupora walirusha risasi mbili hewani na kugeuza gari lao kurudi mjini Arusha lakini wakati wakirudi wananchi waliokuwa karibu na eneo la tukio walitoa taarifa kwa jeshi la polisi na kisha jeshi hilo kufanya jitihada za kuzuia njia zote za kuingilia katikati ya mji wa Arusha.

Alisema kuwa  majambazi hao walipofika katika eneo la Matejoo mjini Arusha walipoona wanafuatiliwa ndipo waliamua kulitekeleza gari walilokuwa wakilitumia na kisha kuanza kukimbia kwa miguu hali iliyopelekea wananchi kuwafukuza na kufanikiwa kuwakamata ambapo waliwapiga kwa mawe na kudai kuwa walifariki dunia wakiwa wanapelekwa hospitalini na polisi

Kaimu huyo alisema  mmoja kati yao alikutwa na bastola aina ya Browning yenye namba 069082  ikiwa na risasi 3 huku 4 zikiwa zimeshatumika.

Alisema kuwa upekuzi uliofanywa na jeshi hilo  ndani ya gari walilokuwa wakitumia majambazi hao walikuta silaha aina ya pump action Mossberg yenye namba R273578 ikiwa na risasi 14 na silaha ya kienyeji aina ya Rifle 458 ikiwa na risasi 3.

Aliwataja wafanyabiashara waliotekwa na kuporwa fedha hizo kuwa ni Silas Soyolo maarufu kama “Mollel”(40),Gregory Joseph(39),Jackson Kisioki(47),Lembris Bikoto(60) pamoja na Jackson Kalaine(35) wote wakazi wa Arusha.

mpwapwa alisema uchunguzi juu ya tukio hilo unaendelea ikiwa ni pamoja na kubaini mmilikiwa gari walilokuwa wakitumia majambazi hao.

Kaimu Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoani Arusha Akili Mpwapwa akionyesha silaha walizokutwa nazo majambazi watatu waliouwawa na wananchi baada ya kupora zaidi ya shilingi milioni nne kwa wafanyabiashara,kushoto ni Rifle 458 iliyokuwa na risasi 3 na kulia ni Pump Action Mossberg iliyokuwa na risasi 14)

Picha na Janet Mushi